... ukawaambie maneno yangu. Ezekiel 3:4

TAFAKARI LA WIKI 10/10/2015


KWANINI ASILIMIA KUBWA YA WATUMISHI WA MUNGU (WAKRISTO) WANAPOANZA KAZI HASA ZA MAOFISINI AU WANAPOHAMIA MAZINGIRA MAPYA KIMAISHA, MAHUSIANO YAO NA MUNGU YANAVUNJIKA?
SOMA PAMOJA NAMI:

Bwana Yesu Kristo apewe sifa!!
Tafakari yetu leo ni muendelezo wa wiki iliyopita.

(Kumbukumbu la Torati 7:1) Bwana, Mungu wako, atakapokutia katika nchi (ardhi) uendeayo kuimiliki, ………….. (Kutoka 34:12) UJIHADHARI NAFSI yako, usije ukafanya AGANO na wenyeji wa nchi ile unayoiendea lisiwe MTEGO katikati yako………………(Kutoka 23:33) kwasababu ukiitumikia miungu yao, jambo hili halikosi litakuwa ni TANZI kwako.” …………… (Kutoka 34:13) Bali utabomoa MADHABAHU zao…….(kutoka 23:25-26) nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, nae atakibarikia chakula chako, na maji yako.Nami nitakuondolea magonjwa kati yako.Hapatakuwa na wenye kuharibi mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako;na hesabu ya siku zako nita itimiliza.

Ukisoma mistari hiyo vizuri katika utulivu kwanamna nilivyo iunganisha, utagundua sababu ambazo biblia imeziweka wazi kabisa, zinazofanya wakristo wengi kupoteza mahusiano yao na Mungu pindi wanapo ingia katika mazingira mapya ki-ofisi au ki-maisha.
Sababu Za Kuvunjika Kwa Mahusiano Na Njia Za Kukuepusha Au Kutatua Uvunjifu Wa Mahusiano Hayo.

Sababu 1 Ni; Kufanya Maagano Na miungu Ya Mazingira Hayo Pasi wewe Kujua:
Unapo fanya maagano na miungu ya maeneo Fulani, ki-biblia maana yake ume halalisha nafsi yako kutumiwa na wao na unakuwa umejiweka kwenye tanzi/mtego ambao kadiri unavyoendelea kuishi katika mazingira hayo itakulazimu kuishi sawasawa na madhabahu zinavyo dai mahali hapo, hata kama hutaki.

Tazama kumbukumbu la torati 7:1-3 na kutoka 34:12, Utagundua kosa kubwa ni maagano ambayo yana vunja uhusino mkubwa katia ya mtu na Mungu, ambayo wakati mwingine mtu anapoingia eneo jipya anayafanya kwa kuto kujua mana hana elimu hii; gafla mahusiano yake na Mungu yanaanza kufifia, ibada zinaanza kukoma kwake, anaiga tabia za wenyeji wa eneo lile au ofisi hiyo,na ukimuuliza sababu za kwanini anafanya vile wakati mwingine hata yeye hazijui sababu,ila amejikuta tu,hajisikii kwenda ibadani mara tu baada ya kuanza kazi, zaidi anajitetea katika namna isiyo na mantiki yoyote.

Natamani ujue moja ya lengo la Daniel ktk kitabu cha Daniel 1:8, kutoshiriki chakula cha mfalme kwa mara ya kwanza kabisa ni kuepuka maagano hayo,
Njia 1, Ya Kutatua Swala La Maagano Ni; Kushughurikia Madhabahu:

Kujifunza kushughurikia madhabahu, kitu cha kwanza unapo fika eneo jipya, jifunze kuchunguza ni Mungu yupi anatawala katika eneo hilo, mfano Paulo ktk Matendo ya Mitume 17:22 alipofika Areopago, aliitazama madhabahu ya mahali pale, akajua ni Mungu yupi watu wapale wana mtumikia, pili alijua kwanini wana tabia za namna ile,kasome vizuri utajifunza zaidi.
Ukisoma 2Wafalme 17:26-33,41 utagundua watu walio hamia eneo lile la Samaria hawakujua tabia za Mungu wa eneo lile, na ndio maana mfalme wa Ashuru alipo ambiwa juu ya adhabu wanazo kutana nazo alisema aende moja ya Makuhani walikuwa Samaria ili akawafundishe KAWAIDA ya Mungu wa eneo lile.

Kuna kawaida za Mungu au miungu katika eneo Fulani, huwezi kuzitambua ila kwa kutazama mahusiano ya wenyeji na madhabahu za mahali pale.
Unapo shughulikia madhabahu ya miungu kwa kuivunja na kusimamisha madhabahu ya Mungu aliye hai, maana yake;-

@kuna miungu unainyima uhalali wa kukutawala,
na unatakasa vitu vya mahali pale kwa lengo la kujinasua kwa mitego iliyokwisha wekwa au itakayo wekwa na kummilikisha Mungu nafsi yako na vyote ulivyo navyo,

@unamruhusu nguvu za Mungu kugeuza fahamu za wenyeji na kuiga tabia zko za ki-Mungu, badala yaw ewe kuiga tabia zao,mfano; Waamuzi 6:25,32
pia unampa Mungu uhalali wa kuwa upande wako na kukutetea kwa lolote pindi unapokutana na upinzani wowote.

@mwisho unakubaliana na uwongozi sawa na tabia za madhabahu ya Mungu inayo kumiliki mahali hapo na kuruhusu hofu ya ki-Mungu kukutawala,kukukumbusha na kukuongoza.

Itaendelea …….
@Daniel Mwaitenga.
Share:
Designed and Developed by Joel Elphas 0757 755 228 or 0655 755 228 © HUDUMA YA GOMBO LA CHUO ...Ukawaambie maneno yangu. Ezekiel 3:4 | ronangelo | NewBloggerThemes.com