TAFAKARI LA WIKI- 04/09/2015
JE, UNAONA NINI?
"Tena neno la BWANA likanijia, kusema, Yeremia, waona nini?....." Yeremia 1:11
Swali la hapo juu (Je unaona nini) linalenga maisha ya pande zote mbili, 1. Maisha Ya Kitumishi....2. Maisha ya kawaida.
Swali ambalo aliulizwa Yeremia lilikuwa ni swali linalohusu Utumishi. Hapa ina maana kuwa, Yeremia alikuwa akionyeshwa picha ya vitu katika ulimwengu wa Roho na kuachiliwa neno kupitia kitu alichoona...yaani UNABII aliokuwa nao.
Katika hali ya kawaida sasa, kama mwanadamu na kama mtumishi.. Unaona nini mbele kupitia Utumishi wako? na Unaona nini kupitia maisha yako ya kawaida?
Kwamfano;
1. Ukiwa umefumba macho alafu unapita juu ya kamba, hutofika mwisho wa kamba, yaani, utadondoka.
2. Ikiwa huna maono yoyote, au mipango yoyote..huwezi kuja kufanikiwa kwa kiwango cha juu.
3. Ukiwa unatamani kuwa kama mtu fulani,utakuja kufikia kiwango cha mtu huyo bila kusonga mbele zaidi, kwa maana umefikia pale ulipoona awali.
4. Ikiwa unaona hatari fulani mbele unapoenda, kwa kawaida utatafuta njia mbadala ili kuiepuka hatari hiyo.
Hivyo, utafika kiwango fulani cha utumishi na mafanikio ya kimwili kwa KADIRI ya unavyoona mbele.
Mfano.. Ayubu hakukata tamaa kwa matatizo na mateso aliyokuwa akipitia, kwa sababu alikuwa akiona mafanikio na matumaini mapya mbele yake.
Je, kwako wewe...UNAONA NINI? KUFELI AU KUFAULU? UGUMU AU WEPESI?
Tembea kwa kuona,kwa maisha yako ya Kiroho na kimwili ili ujue kuwa mwenendo wa safari yako uliyo nayo inakwendaje.