MAMBO YA KUFANYA KABLA
UJACHUKUA MAAMUZI YA MWISHO KWA JAMBO AMBALO LINAKUTESA/LIMEKUCHOSHA KWA KUSHINDWA
KULIPATIA MAJIBU KWA MUDA MREFU.
Bwana asifiwe!!
Kutokana nakuwa tuna MWILI na
DAMU, huwa tunahisi MATESO/MAUMIVU hasa, nyakati ambazo tunapitia mambo magumu
sana,ambayo mara nyingi tunahisi yamezidi IMANI zetu,nyakati hizi kwetu
tunakuwa wapweke na kama tupo katika jangwa, kukosa kuwa na sababu au/na majibu
tunayo yataka ya tunayopitia kuna tupa kuumia,kusononeka,kunung’unika na hatua
inayobaki ni kukata tama kabisa,
Somo la leo ni mambo 3, yatakayo INUA
IMANI yako na KURUHUSU USONGE MBELE; kukwambia kuwa katika mapito hayo Bwana
yupo hapo,haijarishi wangapi wana kupenda au wanakuchukia kutokana na
unachopitia, MFANYE YESU KUWA TEGEMEO LAKO, yani HAKUNA JIBU LOLOTE UNALO
TAMANI, LITAPATIKANA NJE YA MIKONO YA BWANA hatakama limechelewa.
Mf: hujawahi kusikia au kuona mtu
anaamua kutoa rushwa ya ngono ilimradi tu, apate kazi, mana ni miaka mingi
amekaa bila kazi, na jambo hilo lilikuwa mateso kwake. Ni rahisi kumjadili au
kumcheka ilia ukweli ukifunuliwa siri ya yeye kufanya hivyo, unaweza muhurumia
mana hakuwa na msaada hasa maarifa ya IMANI nyakati hizo zaidi ya kupata
anachotaka..madhara yake ni makubwa sasa zaidi ya uwamuzi aloamua kuufanya.
MAMBO YA KUFANYA:
MUHIMU SANA: Usifanye uwamuzi
wowote kwa majira haya hatarishi na ya maumivu kwako, kwa kukosa unacho taka
kwa muda mrefu, ila tumia muda huu sasa
kutulia katikati ya marafiki ambao si
kwazo kwako, mazingira mazuri na ya haki kwako japo kwa wakati fulani ili
ikusaidie…(Zaburi 1:1-4).
A.
KUMSIHI ROHO MT. AKUPE UPENYO UKUMBUKE MAAGANO
ULIYO WAHI KUFANYA KWA KUJUA AU KUTO KUJUA YALIYO MEMA AU MABAYA.
Moja ya mambo yanayo wafunga watu
kukaa kwenye mateso ya muda mrefu yasiyo na majibu ni Agano, mara nyingi watu
huweka maagano kama utani na wakati mwingine pasi kujua; kujua agano ni jambo linalofanya mtu kuvumilia jambo hata
kama jambo hilo majibu yake hayapatikani au yamechelewa, pia linakupa njia ya
kutoka ktk ugumu huo kwa haraka au wepesi zaidi. Liwe ni agano zuri au baya
ambalo umeweka kwa kujua au kuto kujua ni muhimu nyakati hizo kujua mana ni
njia ya kutoka kwa wepesi sana. Kuna mateso yana kutesa au yamekuchosha na
hupati majibu, ila umesahau agano uliloweka.
KUTOKA 32:10-12. Mungu alichoshwa
sana na wana waizraeli, KUCHOSHWA kulimpelekea kuwa na HASIRA, hasira ilimfanya
afanye MAAMUZI MAGUMU sana, lakini RAFIKi yake (Musa) alimsihi maamuzi ya kufanya
kwa kumkumbusha AGANO, kisha Bwana akasamehe,akasahau, akaghairi.
B.
KUOMBA TOBA INAYO LENGA AGANO HILO ULILO FANYA
KWA KUJUA AU KUTO KUJUA, ILI KULIVUNJA KWA AGANO {JIPYA} LA DAMU YA YESU KRISTO,
Ni rahisi sana kupata majibu yetu
kama kuna maagano hasa yale mabaya ambayo yalifanyika kipindi cha nyuma na
nyakati hizi ukumbuki, na unakuta kinachokutesa sasa ni matokeo ya agano lile. Tuna
weza weka maagano kwa namna ambayo tulijua au hatukujua, unapofika kwenye
nyakati kama hizo omba toba juu ya agano hatakama ume likumbuka au la, swala
toba yako ilenge agano, ambayo ni kifungo kikubwa sana katika maisha ya mtu.
C. MBALI NA AGANO, KUJUA SABABU ILIYOFANYA
UKUTANE NA JAMBO LINALO KUTESA SASA, NI MLANGO WA KUTOKA KWA HARAKA KAMA NJIA
ZA MWISHO.
Muhimu sana kufikiri sababu za
jambo hilo kukusumbua na kuzijua njia za kutatua kwa kurudia upya namna
yakupata hatima njema. Sababu na njia hizi zitakusaidia sana kuto kufanya
maamuzi mabaya juu ya swala hilo ambalo limekutesa kwa muda mrefu na kukupa
njia nyepesi ya kupata jibu.
@Daniel Mwaitenga.