SEHEMU YA PILI: NAMNA YA KUJIUNGANISHA NA MUNGU UTOAPO SADAKA
Bwana asifiwe wewe upendwae sana na Mungu
leo tuangalie "mambo ya kuzingatia utoapo sadaka ili kukutana na Mungu."
Kumbuka tu sadaka ni ibada ambayo inakufanya kukutana na Mungu au kuunganisha moyo wako hasa uitoapo sawa sawa na kanuni na utaratibu wa Bwana.
Moja, Fahamu kuwa utoapo sadaka
kinacholengwa ni moyo wako, hivyo ni muhimu sana kuandaa moyo wako kabla
ujafanya maamuzi ya kutoa sadaka. Kumbuka kuwa sadaka si kitu cha kwaida kama
wengi wanavyo weza kufikiri, moja ya mambo yanayoweza kumfunga mtu mikokoni mwa
Mungu au miungu ni sadaka, moja ya kitu kinachoweza kumtoa mtu mikononi mwa
Mungu au miungu na sadaka. “Yeroboamu
akawaza moyoni mwake, “Sasa inawezekana ufalme ukarudi katika nyumba ya
Daudi.Kama watu hawa watapanda kwenda kutoa dhabihu (sadaka) katika hekalu la
Bwana huko Yerusalemu, mioyo yao itamrudia bwana wao, Rehoboamu mfalme wa Yuda.
Wataniua mimi na kurudi kwa mfalme Rehoboamu.’’ Baada ya kutafuta shauri, mfalme
akatengeneza ndama wawili wa dhahabu. Akawaambia watu,“Ni gharama kubwa kwenu
kukwea kwenda Yerusalemu.Hii hapa miungu yenu, Ee Israeli, iliyowapandisha
kutoka Misri.’’Ndama mmoja akamweka Betheli na mwingine Dani.Nalo jambo hili
likawa dhambi, watu wakawa wanaenda hadi Dani kumwabudu huyo aliyewekwa
huko.Yeroboamu akajenga madhabahu mahali pa juu pa kuabudia miungu na kuwateua
makuhani kutoka watu wa aina zote, ijapokuwa hawakuwa Walawi. 1Falme 12:
26-31
Nachotaka uone hapo,
ni njia ambayo Yeroboamu aliitumia ili kuvunja mahusiano ya hawa ndugu na Mungu
aliye hai, alihusisha mambo makuu matatu, mioyo yao, sadaka, na miungu kupitia
madhabahu alizo zitengeneza.Kumbuka kuwa biblia inasema hazina ya mtu ilipo
ndipo na moyo wake utakuwepo, maana yake sadaka inauhusiano mkubwa sana na moyo,
kuna uhusino mkubwa wa maendeleo ya moyo wako na mahusiano ya sadaka unayotoa;
lakini pia
Mbili, Biblia inasema waambie wana
Waisrael wanitolee sadaka kwa moyo wa kupenda, maana yake sadaka ni kipimo cha
upendo wako wako mbele za Bwana, moyoni mwako kuna upendo wa Mungu kwa kiwango
gani; ambacho kitadhirisha utayari wakujitoa kwaajili yake tena kwa furaha kwaajili
ya kazi zake kwa kiwango gani,
Kwahiyo jambo hili
linakupa kujua thamani ya Mungu maishani mwako, ambayo thamani hiyo italeta
msukumo ndani ya moyo wako kutoa sadaka yenye thamani mbele zako na mbele za
Mungu. kwahiyo Roho Mtakatifu anapoachilia msukumo wa wewe kutoa sadaka kiwango
kile anachotaka, moyo uliandaliwa unakupa msukumo kutoa pasipo manung’uniko
yoyote ila kwa furaha katika kile Mungu alicho kukilimia. “Bwana akamwambia Musa,“Waambie Waisraeli waniletee sadaka. Utapokea
sadaka kwa ajili yangu kutoka kwa kila mtu ambaye moyo wake wapenda kutoa.”
Kutoka 25:1-2.
Tatu,
“Kwa imani Abili alimtolea Mungu dhabihu
bora zaidi kuliko Kaini. Kwa imani alishuhudiwa kuwa mwenye haki, Mungu
mwenyewe akazishuhudia sadaka zake. Kwa imani bado ananena ingawa amekufa.Waebrania
11:4
Maana yake sadaka ni
kipimo cha imani na imani ni mlango unaokupa haki mbele za Bwana. Kutoa sadaka
ambayo ni zida kwa upande wako au yenye thamani upande wako na kumpa Mungu ni
kipimo cha Imani yako. Mana Abali, alimpa Mungu vilivyo vinono, Ibrahimu alimpa
Mungu Isaka mwanae wa pekee kama sadaka, Mama mjane alimpa Mungu senti iliyo
onekana kubwa mana ndicho alicho kuwa nacho pekee kama sadaka n.k, kinacho
pimwa hapo ni utayari, na imani waliyokuwa nayo. Ni eneo linalotupa fulsa ya
kujua kuwa tutoapo sadaka, ni lazima kuiunganisha na imani mioyoni mwetu. Toa
sadaka kwa imani kwamba kupitia sadaka hiyo utakutana na Mungu.
Nne,
Sadaka ni kipimo
cha kumcha Mungu, Mungu huifurahia zaka
yako kwakuwa ni sehemu ya heshima unayo muoyesha mbele za macho yake. Thamani
ya sadaka yako inabebwa na kiwango cha uchaji wa Mungu uliyomo ndani yako. Yani
namaanisha hivi, utoapo sadaka Mungu anatazama ni kwa kiwango gani unamcha au
kumuhofu yeye, kwasababu sadaka inatolewa kutokana na kanuni na maelekezo yake,
kwahiyo kitendo cha wewe kutoa sadaka sawa sawa na maagizo yake ni ishara ya
uchaji wako mbele zake, hivyo ni muhimu yeye kupitia sadaka hiyo kukuhudumia
kwa ukaribu zaidi.
“Hakikisheni mmetenga sehemu ya kumi ya mazao yote ya mashamba yenu kila
mwaka.Mtakula zaka za nafaka yenu, divai mpya, mafuta na wazaliwa wa kwanza wa makundi
yenu ya ng’ombe na ya kondoo na mbuzi mbele za Bwana Mungu wenu pale mahali atakapopachagua
kama maskani kwa ajili ya Jina lake,ili kwamba mpate kujifunza kumheshimu/ kumcha Bwana Mungu wenu
daima.” Kumbukumbu 14:22-23
Au
umesahau kuwa Ibrahimu alivyotii kumtoa Isaka sawa sawa na uataratibu wa Bwana
biblia inasema Mungu alimwambi nimejua kuwa unamcha Mungu na sababu hiyo
nitatimiza ahadi yangu juu yako na uzao wako. (Mwanzo 22: 12) Akamwambia,
“Usimdhuru kijana,
wala
usimtendee jambo lolote. Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwa sababu
hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee.’’
Tano, Sadaka kwetu ni ukunjufu wa
mioyo yetu mbele za Bwana, lakini pia ni mlango wa sisi kupokea kwa wingi au
uchache, sawa na tuutoavyo mbele za Bwana “Lakini
nasema neno hili;apandae haba atavuna haba; apandae kwa ukarimu atavuna kwa
ukarimu, ... Mungu humpenda yeye atoaye kwa ukarimu.” 2koritho 9:6-7
Haya ni mambo yanayo
onesha nguvu iliyobebwa kwenye eneo la Sadaka, na mtu akiyazingatia atoapo
sadaka ni lahisi sana kukutana na nguvu za Mungu.
Eneo la sadaka ni pana
sana, na si kwamba unaweza kulitazama kwa jicho moja la upande wa kuunganishwa
na Mungu tu, hapana kama utazamavyo upana huo, yivyo vivyo ni muhimu kutazama
upande wa pili. Upande wa pili ni namna sadaka inavyoweza kuvuruga mahusiano
yako na Mungu. katika ulimwengu tulio nao kama utacheza na sadaka zinazo tolewa
kwa miungu yani waganga na wachawi,maisha yako yana kuwa hatarini sana na ili
ufanikiwe upande huu ni kwanjia ya sadaka. Kwani hujawahi kuona familia inakufa
mmoja baada ya mmoja kwa sababu ya kuotlewa sadaka, na anaefanya hivyo wengine
wafe endapo atakosa sadaka miungu inamuuwa yeye mwenyewe, naamini umewahi
kusikia.
Basi upande wetu tumuaminio
Mungu sadaka nieno la muhimu sana kulijua, si eneo la utani kwa Mungu wetu. Si
kama anashida sana na sadaka zetu, au kapungukiwa, la! Ila analinda na kupenda
sana sadaka maana ni sehemu ya utukufu, na shukurani kwake. Biblia inaweka wazi
AKani alilaaniwa sababu ya sadaka, manabii mianne walikufa kwanguvu iliyopitia
kwenye sadaka, Anania na Safira mkewe walikufa kwa sababu ya sadaka, Akani
alikufa kwa sababu ya vitu vilivyo kuwa vimewekwa wakfu kama sadaka ya Mungu,
Nebukdreza alikolofishana na Mungu kwa sababu hiyo hiyo, na maeneo mengine
mengi ambayo ukisoma biblia utayona yamewekwa wazi. Kwanini sadakja ili vunja
mahusiano ya watu na Mungu kwa upana mkubwa hivyo? ni muhimu ujue kuna siri
kubwa katika sadaka.
Ni sadaka ili muinua
Ibrahimu mpaka kuitwa baba wa Imani,Ni sadaka ya nadhiri iliyo sababisha motto
Samuel akapatikana, sadaka ili mkumbusha Mungu juu yam cha Mungu wake Kornelio,
Sadaka ili pitisha nguvu ya Mungu na kumshindia Elia, sadaka ilikuwa harufu kwa
Mungu pale Nuhu alipoitoa hata Bwana akaweka agano la kutokuuwa kwa mafuriko
ulimwengu mzima. Nachotaka uone ni upana wa eneo hili la sadaka na mimi
nimekufundisha kwa uchache sana kulingana na kipengere alicho nipa Roho
Mtakatifu kukielezea. Lakini nakujengea kiu na msukumo wa kutamani kukutana na
Mungu kupitia sadaka, ndio sadaka inaweza kuinua maisha yako katika Nyanja zote
za maisha yako.
umebarikiwa sana na Mungu.
tutaendelea sehemu ya tatu...........
......."Mambo ambayo uaweza kupokea kutoka kwa Mungu kupitia sadaka"
@Huduma Ya Gombo La Chuo (Daniel Mwaitenga)