UTUKUFU WA MUNGU UNAPOSHUKA, KUTAKA NGUVU ILIYO NDANI YA UTUKUFU HUO IKUSAIDIE WEWE, NI SUALA BINAFSI KATI YAKO NA MUNGU SIO WATU WENGINE, HATA KAMA UTUKUFU HUO UMESHUKA KATIKATI YA KUNDI.
Nimeshuhudia Semina nyingi, Mikutano mingi,matamasha ya Kusifu na Kuabudu, Ibada binafsi au zamakundi nyumbani au makanisani zikishamiri utukufu wa Mungu, lakini utukufu huo hautusaidii kwa kiwango kilicho kusudiwa mana unabaki kuwa ni wa mtumishi aongozae ibada hiyo au wa mahali pale ibada hiyo ilipofanyika, tunashindwa kwenda nao makazini ,majumbani mwetu au kuutumia katika maisha yetu ya kila siku.Nilitoa sababu na naendelea kuzungumza nawe namna tunaweza kukaa mkao ambao tutaufaidi utukufu wa Mungu mahali popote unaposhuka katka maisha yetu ya kila siku.
1.Jifunze kuutambua na tumia NGUVU ya Roho mtakatifu inayoshuka kwaajili ya kukuandaa kabla au wakati wa ibada; nguvu hiyo inakuwa na kusudi na nimuhimu kujua kwanini msukumo wa kujitakasa umeshuka kwa wakati huo, ukiwa barabarani,nyumbani,kanisani,kwenye gari,kazini n.k na nguvu hiyo inataka itumiwe ndani ya muda gani. "Nguvu YA MUDA WA TOBA NA UTAKASO.”
Mbeleni Mungu akinijalia, nitaelezea dondoo hii kwa undani,naamini itakusaidia.
Yoshua3:5 Ndipo Yoshua akawaambia hao watu, “JITAKASENI, kwa kuwa KESHO BWANA atatenda mambo ya kushangaza katikati yenu.”
Hapa Mungu alitaka kujufunua kwao si kwa mazungumzo la! Ila alitaka kwa kushusha utukufu wake awavushe mto yordani, ukiona Mungu amewapa masaa 24 ya kujitakasa ujue kuna sababu.
2. Nimuhimu sana, kufahamu kuwa unapoingia kwenye ibada unatakiwa kujiunganisha moyo wako na Madhabahu ya Mungu, na Mungu mwenyewe na Ufalme wa Mungu uliozamu kushuka na kuhudumia ibada hiyo.
Tazama kosa walilofanya hawa ndugu, la kijiunganishi na watumishi wa Mungu badala ya kujiunganisha na Mungu; Utukufu wa Mungu uliposhuka Ibada ikaisha wao wakabaki waanajadili lile wingu na kufikiri ni kina Paulo walifanya vile na kutaka kuwasujudia na kuwainua wao, jua,hawakufaidi chochote mpaka walipokemewa na kufundishwa,
Tazama Elimu ya kiroho MT.Paulo aliyowapa:-
Matendo ya mitume 14:15 “Enyi watu, kwa nini mnafanya mambo haya? Sisi ni wanadamu tu kama ninyi! Tunawaletea habari njema, tukiwaambia kwamba mgeuke mtoke katika mambo haya yasiyofaa mmwelekee Mungu aliye hai….”
3. Unapogundua utukufu wa Mungu umeshuka kwako katika namna ya pekee, jifunze kujiungamanisha na utukufu huo kwa SADAKA. Hiyo ni alama na njia inayolazimisha utukufu huo kukufuatilia hata baada ya ibada hiyo.
Waamuzi 6:18-22. 18 Tafadhali ninakuomba usiondoke hapa mpaka nitakaporudi na kukuletea sadaka yangu na kuiweka mbele yako.’’ Naye BWANA akamwambia, ‘‘Nitangoja mpaka utakaporudi.’’ Tumia SADAKA hiyo kuzungumza na Mungu- Mwanzo 18:1-8 Abrahamu akainua macho akaona watu watatu wamesimama karibu naye. Alipowaona, aliharakisha kutoka kwenye ingilio la hema lake kuwalaki na kuwasujudia hadi nchi. 3.Akasema, “Kama nimepata kibali machoni penu, ee bwana wangu, usimpite mtumishi wako. 4Acha yaletwe maji kidogo, kisha ninyi nyote mnawe miguu yenu na mpumzike chini ya mti huu. 5Niruhusuni niwapatie chakula kidogo mle, ili mpate nguvu mwendelee na safari yenu, kwa kuwa mmekuja kwa mtumishi wenu.’’ Nao wakamjibu, “Vema sana, fanya kama unavyosema.’’
4. Wakati huo utukufu wa Mungu unashuka, omba roho ya Mungu iliyomo ndani ya huo utukufu ikae juu yako, kabla hujafikiri kuomba mahitaji yako. Hesabu 11:25, 2Falme 2:9. “…Elisha akajibu, “Naomba nirithi sehemu maradufu ya roho yako.’’ Kumbuka ndugu; kitendo cha Elisha kuomba ile roho si roho ya Elia ila roho wa Mungu aliye kuwa juu ya Elia. Vivyo hivyo roho ya Mungu iliyo kuwa juu ya Musa kwa wale watu 70. Sasa kumbuka mabadiliko makubwa ambayo yalifanyika pindi roho hiyo ilipo kaa ndani yao.
5. Uwe mwenye
kutamani kusikia na kuelewa/kujua na kuamini ujumbe uliobebwa kwenye huo
utukufu; utukufu wa Mungu ukishuka
unakuwa na ujumbe au sababu ya kushuka hapo; kumbuka neno la Mungu ndio ujumbe
unaobebwa katika utukufu huo, ndio majibu yanayokujia,na ndio hatua ya imani
yako. na maadamu ukiamini umeshuka mahali ulipo lazima ujue unakuhusu na
wewe.5. Weka IMANI kubwa kwa Mungu
aliyejifunua hapo na kwa yale unayoenda
kuyaomba.
Marko 9:22-24 …………………Lakini kama
unaweza kufanya jambo lo lote, tafadhali tuhurumie utusaidie.’’ 23Yesu
akamwambia, “Kama ukiweza kuamini, yote yawezekana kwake yeye aaminiye.’’24Mara
baba yake yule mvulana akapiga kelele akisema, “Ninaamini. Nisaidie kutokuamini
kwangu!’’
7. Achilia mahitaji yako kwa kadiri Roho Mtakatifu anavyo
kusukuma kuomba, kwa lugha nyepesi huo ni muda mzuri wa kujiachia kuzungumza na
Mungu, mana amejifunua, Roho Mtakatifu anaweka ajenda za muhimu,za lazima na za
muda sahihi ndani yako zinazo kuwa na mahusiano makubwa na maisha yako ya sasa
na baadae katika kusudi uliloumbiwa (future yako) ambazo ni muhimu uzungumze na
Mungu kwa mzigo na msukumo wa maombi mahali hapo. Kumbuka habari za Bartimayo
Kipofu, mama mwenye kutokwa damu miaka 12
(Marko 5:25-34), Musa alivyo kuwa anajiachilia mbele za Bwana na taifa
lake pia (Kutoka 24:10-25).
8. Ili kumiliki utukufu wa Mungu ulioshuka,hasa ukusaidie
baadae, jitahidi sana kuwa mchunguzi wa neno la Mungu na mtii wa kila utakacho
kielewa kwa kwa kukitenda Hivyo ni muhimu wingu hilo unapofika katika utulivu
kuwa mchunguzi wa neno lililo achiliwa wakati huo.
Matendo ya Mitume 17:11-12 “Hawa Wayahudi wa Beroya walikuwa
waungwana zaidi kuliko wale wa Thesalonike,kwa kuwa walilipokea neno lile kwa
uelekevu wa moyo,wakayachnguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo
ndivyo yalivyo 12Wayahudi wengi wakaamini pamoja na wanawake na wanaume wa
Kigiriki wa tabaka la juu.”
@Daniel Mwaitenga.
Huduma Ya Gombo La Chuo.