HUDUMA YA GOMBO LA CHUO:
Haleluya Ndugu Yetu Katika Krsto Yesu!
Tuna furaha kwaajili yako,tunatamani walau ujue kwa sehemu dhumuni la HUDUMA YA GOMBO LA CHUO.
Lengo la Huduma
Hii ni huduma isiyofungamana na
udhehebu au udini, yenye lengo la kuhubiri injili ulimwenguni sawa na agizo la
Mungu wetu kwa Kristo Yesu “Marko 16:15”.
Ezekiel 3:4 “... uwaambie maneno yangu.”
Mungu ametupa mstari huu
uliobeba huduma hii,ambao unaunganisha Moyo wa Huduma hii(wahudumu),moyo wa
Mungu mwenyewe na mioyo ya watu tunao wahudumia kwa uweza wa Roho Mtakatifuwake
na katika Kristo Yesu
Makao makuu: Makao makuu ya Huduma ya Gombo La Chuo yanapatikana
Mwanza –Tanzania.
Imani Yetu:
Tuna amini, imani moja inayowaunganisha wakristo ulimwengu kote. Mungu Baba, Mungu Mwana(Yesu Kristo), na
Roho Mtakatifu. Na Biblia takatifu yenye vitabu 66, ndio msingi wa mafundisho
yetu.
Karibu:
Ungana nasi kwa
MAOMBI na SADAKA yako au njia yoyote
ambayo Mungu amekujalia ili tuujenge
mwili wa Kristo.Ubarikiwe.
na
Uwongozi wa Huduma Ya Gombo La Chuo