... ukawaambie maneno yangu. Ezekiel 3:4

UHAI WA NENO LA MUNGU NDANI YA MKRISTO 

UHAI WA NENO LA MUNGU NDANI YA MKRISTO 


Efeso 1:15.......
Mtu aliye nakiu yakujua uzuri wa Mungu na siri yamaisha yake ndani yakristo, imempasa kuyajua haya
Kama ilivyo ktk maisha yakawaida, sheria ndio msingi na mwongozo ktkt ya watu wawili, familia, jamii, taifa hata ulimwengu mzima na haki ndio uhuru na furaha ya mtu,haijalishi ufukara au utajiri alionao ila haki ni nguvu ya utetezi na amani , ndivyo ilivyo ktk kristo, sheria ndio inatupa kujua namna tunaweza mpendeza Mungu na kuishi nae kwa uzuri zai, lakini haitusaidii pale tunapo mkose, ila damu ya Yesu kristo pekee utusaidia kupata haki itupayo uhuru, furaha na ninguvu ya amani; yaani injili.
Ktk maisha ya kikristo, Uhai wa Neno la Mungu ndani mtu, ndiyo jambo la Muhimu kuliko vyote.

Kuijua injili na sheria ndio uhai wa Neno la Mungu ndani ya mtu, huwezi kuvitenganisha vitu hivi viwili, na  huwezi kutafuata kuukulia wokovu kama unatenganisha hivi. 

Ktk kimoja dhambi hudhihirishwa na kwa kingine dhambi husamehewa/huondolewa.



tofauti hii ni ufunguo wa kulielewa Neno la Mungu – Biblia Takatifu – na ufunguo wa kumfahamu Mungu.


Watu wengine wanadhani kwamba Sheria ni Agano la Kale, na Injili ni Agano Jipya. Lakini si kweli! Katika Agano la Kale na Agano Jipya tunakutana na Sheria na Injili.


" “Tofauti kati ya Sheria na Injili ni kubwa na nuru kubwa. Kwa kuona hivyo Neno la Mungu litagawanyika sawa, na maandiko ya manabii watakatifu na mitume yatatangazwa na kuelezwa sawa.”

Tunapohubiri, lengo letu ni kulifanya Neno la Mungu kuwa hai ili kila mkristo apate kukutana na Mungu. 
"Lengo la mahubiri na mafundisho yote ni watu wapate kukutana na Mungu.(Mungu pamoja nasi)

Lakini Mungu ni wa namna gani? Ikiwa nitawaeleza wengine jinsi Mungu alivyo, lazima kwanza nimjue mimi.”


SHERIA

Sheria ya Mungu inaonyesha mapenzi ya Mungu. Ni jinsi anavyotaka tuishi vizuri pamoja. Sheria inalenga moyo wangu, kazi yangu na matendo yangu.
Sheria ni yale yote Mungu anataka niyafanye.

Hapa unaona kwamba Mungu ni Mtakatifu. Kwa hiyo aliwaamuru: “Mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wenu, ni mtakatifu.” Walawi 19:2.


Dhambi inaleta hasira ya Mungu.
Mwenye dhambi hawezi kumwona Mungu na kuishi.
Amri ya Mungu kwa ajili yetu:
“Kwa ajili ya hayo mtazishika amri zangu na hukumu zangu; ambazo mtu akizitumia ataishi kwa hizo; mimi ndimi BWANA.”  Walawi 18:5.
Hukumu ya Mungu:
“Na alaaniwe asiyeyaweka imara maneno ya torati hii kwa kuyafanya. Na watu wote waseme, Amina.”  Kumbukumbu 27:26.

Watu waseme amina kwa sababu Sheria ni nzuri

Sheria ni nzuri na takatifu, yenyewe hutangaza mapenzi ya Mungu
Ni mafundisho na mwongozo, yani maneno yatokayo ktk kinywa cha Mungu.


Hakuna kosa kama hakuna sheria Rumi 4:15”

The Law showing sin in my heart and The Gospel – showing the mercy in God’s heart


Huongoza ibada zote na matendo yote ya watu wa Mungu,wanao Kubali kumtumikia na kulishika agano lake.
Sheria huangaza roho, ila sheria haitoi nguvu ya kushinda dhambi.




 Sababu hiyo torati imekuwa kiongozi wa kuwapeleka watu kwa kristo.Galatia 3:22-25.

Lazima kanisa lijue kuwa sheria imekufa kwa upande mmoja au kufishwa nguvu,Lakini si kwa namna yakuto kutambulika.

Yesu hakuja kuitangua sheria ila kuitimiliza, Mathayo 5:17”

Na upande mwingine Yesu hakuja kuitangua torati ila kuitimiliza,maana yake, katoa nguvu ya roho yake kuishinda dhambi.
Nguvu mpya umetolewa kwa mtu, ilikuyatimiza yote yaliyonenwa kwenye torati.


Warumi 8:2-4 “ …ilimaagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi..”


Wakati tofauti kati ya Sheria na Injili haitambuliwi katika mahubiri na mafundisho, Neno la Mungu litakuwa kivulini, na mtu atakuwa na mashaka kama kweli ameokolewa na Yesu tu.


Lazima kanisa lijue kuwa sheria imekufa kwa upande mmoja au kufishwa nguvu,Lakini si kwa namna yakuto kutambulika.
Yesu hakuja kuitangua sheria ila kuitimiliza, Mathayo 5:17”

Na upande mwingine Yesu hakuja kuitangua torati ila kuitimiliza,maana yake, katoa nguvu ya roho yake kuishinda dhambi.
Nguvu mpya umetolewa kwa mtu, ilikuyatimiza yote yaliyonenwa kwenye torati.


Warumi 8:2-4 “ …ilimaagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi..”
Sheria inatuhusu nini? 


Mioyo yetu imejaa na dhambi. Matokeo ya jambo hili ni kwamba nia yetu ya kuitimiza Sheria imepotea. Unaona sasa! Kwa sababu mimi ni mwenye dhambi moyoni, natenda dhambi.

The Law show us our sin but can not take it away from us.
Sheria ni neno kuhusu kuhukumiwa, neno kuhusu hasira, neno kuhusu huzuni na maumivu, neno kutoka kwa hakimu ya kuhukumu, neno kuhusu kuogopa, neno kuhusu laana. Kupitia Sheria hatupati cho chote ila dhamiri mbaya, moyo unaosumbuliwa, roho ya hofu. Sheria inatuonyesha dhambi zetu, lakini haiwezi kuziondoa.”

Hii ndiyo hali yetu mbele za Mungu!


Mawazo fulani:

1.Bila sauti ya Sheria hakuna anayeona kwamba anahitaji
   Injili.

2. Mkristo anahitaji kuona jinsi alivyo Mungu. Ni Mtakatifu,
    mwenye enzi yote, mwenye upendo na mengine
    mengi…. Kuhubiri Sheria ni kuonyesha jinsi Mungu
    alivyo.

3. Mkristo anahitaji kujifunza mapenzi ya Mungu, jinsi
    anayependa tuishi.

  4. Mkristo anahitaji kujifunza na kujua jinsi alivyo
    mbele za Mungu na Sheria.

5. Mkristo anahitaji kujua kwamba anamhitaji
    Yesu kuwa Mwokozi  wake. Kujiona kuwa
    mwenye dhambi, na hii ni sababu anatenda
    dhambi.

6. Utakumbuka kusoma Biblia katika nuru ya
    Kristo. Kujua tofauti kati ya kuwa ndani au
    nje, kuishi au kutokuishi na Kristo.

7. Kuhubiri Sheria si sawa na sauti ya ngurumo (=
    hukumu). Wakati Yesu alihubiri neno la Sheria
    na hukumualiulilia mji wa Yerusalemu na
    watu wake.

8. Kumbuka kila wakati kwamba matendo ya
    mwanadamu hayawezi kumletea wokovu. Kwa
    hiyo ni kosa kuhubiri Sheria peke yake.


Mahubiri ya kikristo ni Sheria pamoja na Injili.

Injili ni nini?
Sheria unaweza kufahamu na kuelewa kwa akili zako.
Tofauti na Injili. Injili ni bila sababu.


 Injili ni ”Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu), Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.” 1. Kor. 2:9.

UPANA WA INJILI
Injil ni Neno pana sana,
RUMI 1;16 “…injili niuweza(nguvu ya) wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye,…….”
Kupitia kifungu hicho utakubaliana namimi kuwa injili ni neno pana sana, Mana uwezo au nguvu za Mungu hazikomei kuelezewa katika uzima wa milele tu, ila kusudi lake ni kufikia kikomo cha uzima wa milele.
Injili ni msamaha na neema ya Mungu. Kwa neema yake Kristo ananiokoa na hasira ya Mungu.

Injili imepunguzwa kwa kiwango kikubwa sana, pindi inapo hubiriwa.
    Imepunguzwa na kuwa si injili ya UFAMLE bali ni injili ya WOKOVU tu.
Lazima ihubiriwe kwa namna ya utu wa mtu wote na mazingira yake yote, duniani kote  (maisha baada ya wokovu duniani na mbinguni nasio mbinguni tu).
Mungu anapo muumba mwanadamu alimtengenezea mazingira kwanza, lazima ujue hilo Mwanzo 2;5,15),
kumbe tunapo zungumzia injili ya wokovu ni lazima tugusie mwanadamu na mazingira pia.
 Wakolosai 1;19-20
kwakuwa ktk yeye ilipendeza utimilifu wote ukae. Na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake, akisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye ikiwa nivitu vilivyo juu ya nchi au mbinguni”.
Rumi 8;19-21
“kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu. Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili, si kwa hiari yake, ila kwasababu yake yeye aliyevitiisha ktk tumaini.


    kwakuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa ktk utumwa wa uharibifu, hata viingie ktk uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu
Fikia kiwango cha kutambua maana ya ujio wa Yesu kristo.
Mathayo 1:23, inaeleza maana ya ujio wa kristo, yakwamba Mungu ameshuka kukaa pamoja nasi hapa duniani na milele, na hiyo ndio injili yaani habari njema.
Habari njema ni ujio wa ufalme wa Mungu,sawa na mathayo 4:17.


Ukifuatilia Mathayo 13, utakutana na mifano mbalimbali,  mitano kati ya hiyo, inatupa picha ya ufalme wa Mungu hapa duniani na miwili ni ufalme wa Mungu mbinguni.



linaendele Mungu akusaidia kuelewa........efeso 1;15..

Share:

Related Posts:

Designed and Developed by Joel Elphas 0757 755 228 or 0655 755 228 © 2025 HUDUMA YA GOMBO LA CHUO ...Ukawaambie maneno yangu. Ezekiel 3:4 | ronangelo | NewBloggerThemes.com