MUNGU ANAPOTAKA KUJIFUNUA KWAKO, ROHO MTAKATIFU ANATABIA YA KUMUANDALIA MAZINGIRA NDANI YAKO NA KUKUANADAA WEWE ILI USTAHIMILI KUUPOKEA UTUKUFU WA MUNGU ANAPOSHUKA KWA KUKUFUNDISHA KUHESHIMU NA KUTUMIA “NGUVU YA MUDA WA TOBA NA UTAKASO.”
Bwana
Yesu Kristo Asifiwe!!!
kama
Raisi katika maisha ya kawaida
kabisa anavyo andaliwa mazingira ya eneo analo taka kwenda,ziara hiyo
yawezekana ameombwa kwenda au ipo katika mipango yake. na watu wakumpokea
wanavyo andaliwa namna yakustahimili kumpokea na kumfaidi kwa ule ujio wake;
vivyo hivyo katika maisha ya kiroho kuna maandalizi.
Ni rahisi sana kumuomba
Mungu ajifunue katika maisha yako, lakini ni vigumu sana kwa wengi kuwa na
maandalizi au kujua ni namna gani Roho
mtakatifu anaachilia fulsa/mwanya wa kujiandaa ili kumruhusu Mungu kujifunua
ndani yako wakati atakao yeye.
Swala
la utukufu wa Mungu ni kitu binafsi kati ya Mungu na wewe, na wala si kundi
hata kama utukufu huo umeshuka kwenye kundi.
Umewahi kujiuliza
kwanini watu wengi katika mikutano ya injili, ibada za makanisani au katika matamasha
ya kiroho utukufu wa Mungu unaweza kushuka na usiwasaidie kabisa,hata kama
mtumishi yupo vizuri, wataouna hapo na wengi nguvu zile zitawadondosaha, ila
hawaendi nao popote, mkutano au semina ikiisha na wao wanarejea katika hali ya
kawaida.
Au umewahi kujiuliza
kwanini Mungu anaweza kushuka sehemu, alafu wewe upo lakini yeye akaondoka kwakusema
haupo, Tazama vifungu hivi walau kwa uchache unielewa nacho maanisha; Mwanzo 3:9 Isaya 50:2, 65:12, 66:4 na
Ezekiel 22:30.
Moja ya tatizo ni
maandalizi yaliyo fungwa ndani ya MUDA wa TOBA na UTAKASO.
Sasa najua Roho
mtakatifu ameamua kutuvusha hapo,kwa kutusaidia kujua na kutumia NGUVU iliyomo
ndani ya Muda wa Toba na Uatakaso..
Fuatana na mimi utaelewa
zaidi.
Matendo 3:19 TUBUNI
basi (mrejee) MKAMGEUKIE Mungu, ili dhambi zenu zifutwe, ili zipate kuja
nyakati za kuburudishwa kwa kuwepo kwake Bwana
Toba tunafanya ili kugeuga kama tupo katika njia isiyo
sawa basi turejee kwa Bwana, na toba hiyo inabebwa sana na muda.wengi wanaweza
kuwa hawajui hilo mana lazima ujue ukicheza na toba unacheza na ufalme wa
mbinguni, vitu hivi viwili vinabebwa na muda
Tazama Mathayo
3:2“Tubuni,
kwa maana Ufalme wa Mbinguni u karibu (muda).”
Utakaso
tunaufanya kwa lengo la kuwekwa wakfu
kwa kazi ya Bwana, tunafanya kwa kututenga
rasmi kwa kazi au mazungumzo na Bwana, tunafanya kwa kuweza kustahimilishwa walau kuuona utukufu wa
Mungu na kusikia anaujumbe gani kwetu, lakini zaidi kustahimili kuupokea
kilicho bebwa ndani ya utukufu huo kila siku ajifunuayo ndani yetu.
Lengo la utukufu wa
Mungu kushuka;
ni kukuvusha eneo ulilo kwama au
kukupeleka eneo lililokusudiwa. Ni ishara/alama kwamba nguvu za Mungu zipo na
wewe, ulionekana ukivusha watu mto yordani…jifunze pia uhusiano uliopo kati ya
Yoshua 3:5 na Yoshua 7:13….utukufu huu uliwavusha hawa ndugu, haukuwavusha tu
ukakoma la! Ila ulikuwa pamoja nao, ila walipotenda dhambi utukufu wa Mungu
ukaondoka, wanao jua kupima mizani ya kiroho walipoona haupo wakamuuliza Mungu
kosa liko wapi, walipo liona kosa na kutengeneza kwa kuheshimu muda wa toba na
utakaso ambao ulihusisha KABILA,JAMAA,FAMILIA HADI MTU BINAFSI, utukufu
ukarejea na wakazidi lutembea na Mungu. Ni kitu cha mtu binafsi hatakama
kimeshuka kwa watu wengi.
Kuna vitu vinadhihirisha kuwa hapa utukufu wa Mungu niliye anzanao upo, umepungu,umeongezeka
au umeondoka kabisa… ukijua kutumia muda wa toba na utakaso inakusaidi kujua
tatizo ni nini na nini la kufanya. Tazama Yoshua 3:5,7:13, Kutoka 19:10, 24:16
13:21, 40:34 1Falme 8:10, Yohana 1:14, Ufunuo 15:8…n.k
Tazama 1:
Kutoka 19:10 Naye BWANA akamwambia
Musa, “Nenda kwa watu ukawaweke wakfu (ukawatakase) LEO NA KESHO…..11 na wawe TAYARI KATIKA
SIKU YA TATU, kwa sababu siku hiyo, BWANA atashuka juu ya mlima Sinai machoni
pa watu wote.
Hapa Mungu alitaka
kujifunua si kwasababu wametenda dhambi la! Ila alitaka kuzungumza nao, Swali
linakuja kwanini aliwaambia wajitase ndani ya masaa 48?
Mfano:- umewahi kuwa
njiani au kwenye gari,kazini au popote pale gafula unasikia kuomba maombi ya
toba na kujitasa? Alafu ukapuuzia au
ukasema ntaomba baadae au ntaomba nyumbani
au ntaomba kesho, na uwo muda uliopanga wewe ukaomba kiu ya kuomba
ikakatika au usiombe kwa shauku na mzigo ambao ulikujia pale ndani?
Sasa najua wengi
watasema ningeombaje kazini? Hilo ndio kosa la kwanza kushindwa kujua namna ya
kuomba maombi ya namna tofauti mahali tofauti hasa kwa kushindwa kuwa na
maana(definition) nzuri ya maombi ni nini.
Kosa la pili litakuja
kwa kushindwa kuutumia ule muda, ambao nguvu zake ni matokeo ya nini Mungu
alitaka kufanya kwaajili yako, na pia nguvu zake ndio sababu iliyo mfanya Roho
Mtakatifu kukuheshimu, kukupenda na kuja kukuandaa..
Tazama 2:
3:5 Ndipo
Yoshua akawaambia hao watu, “JITAKASENI, kwa kuwa KESHO BWANA atatenda mambo ya
kushangaza katikati yenu.”
Hapa Mungu alitaka
kujufunua kwao si kwa mazungumzo la! Ila alitaka kwa kushusha utukufu wake
awavushe mto yordani, Swali linakuja kwanini aliwapa masaa 24 ya kujitakasa?Yoshua
Mungu atupi vitu eti
kwasababu tu, tulimuomba, ila wakati mwingi anatoa kulingana na mipango aliyo
kuwa nayo hasa kuzingati muda aloukusudia. Lakini wewe kupokea ndio hasa
inategemea mazingira uliyopo,
Tazama 3:
Yoshua7:13 ‘‘
‘Nenda, ukawaweke watu (uwatakase) wakfu. Waambie, ‘JITAKASENI mjiandae kwa
KESHO, kwa sababu hili ndilo asemalo BWANA wa Israeli: kwamba kitu kilichowekwa
wakfu kipo katikati yenu, Ee Israeli. Hamwezi kusimama dhidi ya adui zenu mpaka
mtakapokiondoa.”
Hapa Mungu taifa la Isrel lilienda kinyume na agano walilo weka na Mungu, mmoja wao alipokosea Mungu akanyamaza kimya wakapigwa na adui zao, Yoshua alipoomba toba na kumuuliza Mungu, Mungu akawapa muda wajitakase ili ashuke na alitatue tatizo Swali langu kwanini aliwapa muda ule tena wajitakase?
Jiulize na Wewe!!
1. Je, wasingekuwa wanatumia ndani ya masaa hayo
wanayopewa kujitakasa nini kinge kuwa kinatokea? Na kama umeona walau ka upenyo
kakujibu swali, umeina nguvu iliyobebwa ndani ya muda huo wa kujiweka wakfu?
2. Kwanini Biblia haijaweka wazi sana juu ya watumishi
wa Mungu ambao wamekuwa na mazungumzo na Mungu kila wakati, kama Ibrahimu,
Yakobo, Musa, Yoshua….n.k?
Jibu
langu fupi tu, ni moja ya
vitu ambavyo Mungu amenifundisha; watu hawa walikuwa na uwezo mkubwa sana
wakutembea kwa maelekezo ya Roho mtakatifu hasa kwa kuheshimu muda huo wa toba
na utakaso.
Kuna maandalizi binfsi ambayo Roho Mtakatifu anamuandaa mtu pale Mungu
anapotaka kujifunua kwa mtu huyo pasi kujarisha anajifunua kwa ghadhabu au wema,
ila jua hili; ukimpa Mungu nafasi ndani yako, ukakubali kutembea chini ya agano
la kristo, utakapo kosea njia kwa kuifuata ile iliyo kinyume na Kristo, Mungu
yupo tayari kuingilia kati, au ukiwa chini ya uangalizi wa Kristo,tayari upo
kwenye nafasi ya Mungu kujifunua au kukuhudumia wakati wowote apendao; lakini kabla ya hayo mawili kutokea, Roho Mtakatifu
anakuandaa kuruhusu hali ya Mungu kuingilia kati.
Lengo langu ujifunze kitu hiki; maandalizi ya Roho mtakatifu huwa yana
tazama sana MUDA na sio mazingira, nini Mungu amekusudia kufanya kwako wakati
fulani ndiocho kitu kinacho mpa Roho Mtakatifu nafasi ya kuku andaa mapema sana.
@Daniel Mwaitenga
Huduma Ya Gombo la Chuo