... ukawaambie maneno yangu. Ezekiel 3:4

SEHEMU YA KWANZA: NAMNA YA KUJIUNGANISHA NA MUNGU KUPITIA SADAKA

NAMNA YA KUJIUNGANISHA NA MUNGU UTOAPO SADAKA.
Bwana asifiwe!!
Naamini upo tayari nikuletee somo hili,
Basi neema ya Yesu Kristo, Upendo wa Mungu Baba na Ushirika wa Roho Mtakatifu ukufunike,
Tutaangalia mambo makuu mawili
  1. Mambo ya kuzingatia utoapo sadaka ili kukutana na uwepo wa Mungu kupitia sadaka hiyo
  2. Mambo unayoweza kukutana nayo, kupata au kupokea utoapo sadaka. 

UTANGULIZI:
Nikweli kwamba 
moj; kushindwa kuona faida na maana ya kutoa sadaka kumesababisha Wakristo wengi kushindwa au kuchelewa kupokea mambo ya rohoni na mwilini sawa sawa na neno la Mungu liahidvyo, kwani si wengi wanapokea matunda ya kile wanachokitoa. Wengi wanajitahidi kutoa lakini bado milango haifunguki, kwa hiyo wanakuwa na maumivu mioyoni mwao nakukata tamaa kwenye eneo la utoaji,
Kitu cha pili wengi wanaamini sadaka wanayotoa wanakula watumishi au watu au inawatajirisha watumishi na wala haiendi popote, hasa wanapokutana na ugomvi unaotokana na sadaka makanisani n.k, kwa hiyo mzigo au msukumo wa kutoa sadaka miyoni mwao ni mdogo na kupelekea kutoa kama mazoea mana mioyoni mwao wanamtazamo na imani yakuwa zinaenda mifukoni mwa watu.

Nimuhimu sana ujue jambo hili, uwendapo mbele za Bwana ilikutoa na kupokea kuna kanuni na utaratibu wa Mungu mwenyewe ambao ni lazima ufahamu kinyume na hapo utoaji wako bado utakuwa na hasara, na mateso au maumivu ya upotevu wa mali yako. kweli bara tuelezane ukweli kuliko kukuacha utoe bila faida, hata neno la Mungu limeweka wazi jambo hili.

Lakini kadili unavyo soma kipengere hiki kuna ufahamu mpya Mungu atakusaidia kujua eneo hili, sadaka ni ibada kati yako binafsi na Mungu. Eneo la sadaka ni jambo la siri na binafsi kati yako na Mungu, kutoa sana au kidogo, kutoa kwa mchungaji au mtumishi Fulani bado havikusaidii kama ufahamu wako utaishia kujadili mambo hayo na kuyapa nafasi katika moyo wako.Lakini kulenga dhamira ya moyo wako sadaka unayotoa inaenda wapi na kwa nani (mtu au Mungu), imani yako katika sadaka utoayo, na uwaminifu wako mbele za Mungu ndio maana halisi ya sadaka yako. Kwa namna hii, naamini Mungu anataka ujue eneo la utoaji lilivyo na nguvu, lilivyo la muhimu na linavyoweza kukuunganisha na Mungu.

 Sijui kama unajua jambo hili, kuwa moja ya maeneo ambayo yanaweza kukuunganisha moyo wako au kukutoa mikononi mwa Mungu au miungu ni sadaka; pia ni eneo linaloweza kujenga au kuharibu mahusiano yako na Mungu au miungu. Awe ni Mungu au miungu pande zote hutaka na hutolewa sadaka, na maeneo yote yana kanuni amabazo zinataka kufanana.

Tufuatane pamoja kwa kusoma neno la Mungu, uone nacho zungumza nawe; Malaika wa Bwana alipomtokea Gideoni, akamwambia, “Bwana yu pamoja nawe, Ewe shujaa mwenye nguvu.” Gideoni akajibu, “Ee Bwana wangu, kama Bwana yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametutokea? Yako wapi basi yale matendo yake makuu baba zetu waliyotusimulia juu yake waliposema, ‘Je, Bwana hakutupandisha kutoka Misri? Lakini sasa Bwana ametuacha na kututia katika mkono wa Midiani.” Bwana akamgeukia na kusema “Enenda kwa uwezo wako huu, ukawaokoe Israeli kutoka mkononi mwa Wamidiani. Je, si mimi ninayekutuma wewe?’’ Gideoni akauliza, ‘‘Ee Bwana wangu, nitawezaje kuwaokoa Israeli?Ukoo wangu ndio dhaifu kuliko zote katika Manase, nami ndiye mdogo wa wote katika jamaa yangu.’’ Bwana akamjibu, ‘‘Nitakuwa pamoja nawe, nawe utawapiga Wamidiani kana kwamba walikuwa ni mtu mmoja.’’ Gideoni akajibu, ‘‘Kama basi nimepata kibali machoni pako, nipe ishara kuonyesha kweli kwamba ni Wewe unayesema nami.Tafadhali ninakuomba usiondoke hapa mpaka nitakaporudi na kukuletea sadaka yangu na kuiweka mbele yako.’’Naye Bwana akamwambia,‘‘ Nitangoja mpaka utakaporudi.’’ Waamuzi 6:12-22.

Natumai umewahi kuzisoma habari za Gidion zinazopatikana Sura hiyo ya 6, Lakini muhimu kwangu nataka tujue kwamba, wakati Mungu anamtokea Gidion, taifa la Israel lilikuwa mikononi mwa adui zao ambao ni Wamidiani. Taifa la Israel walikuwa wakivuna mavuno yao Wamidian wanachukua na mateso mengi waliyapitia mikononi mwa hao adui zao. Inawezekana na wewe unapita katika matatizo magumu, lakini kwanza nataka ujue wana waisrael walipita katika wakati mgumu sana, kosa lao lilikuwa ni kumuacha Mungu, Kumuasi na kutumikia miungu mingine, kwa muda mrefu Mungu aliwanyamazia kimya.

Mungu alipokusudia tena kuwarudia alijifunua kupitia kijana mmoja aliyekuwa wa familia iliyokuwa masikini na alikiuwa ni mtoto wa mwisho. Jambo kubwa lililokuwa katika ufahamu wa Gidioni ni kwamba, aliwahi pewa habari za ukuu wa Mungu jinsi na namna alivyo wakomboa baba zake kutoka Misri. Na swali kubwa alilokuwa nalo, ambalo nahisi ilikuwa ni shauku yake kuwa siku Bwana akitokea nita muuliza, na kweli sikumoja Mungu alijifunua mbele ya macho yake, Gideoni akasema, “Ee Bwana wangu, kama Bwana yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametutokea? Yako wapi basi yale matendo yake makuu baba zetu waliyotusimulia juu yake waliposema, ‘Je, Bwana hakutupandisha kutoka Misri? Lakini sasa Bwana ametuacha na kututia katika mkono wa Midiani.” (Waamuzi 6:12)
Ni ukweli wa dhati kuwa,kama umewahi sikia kwa watu kuwa Mungu anafanya mambo makuu lakini kwa wakati wako huyaoni na unateseka utakuwa na maswali zaidi kuhusu Mungu ukihusianisha na hizo habari ulizo ambiwa,ndivyo ilivyo kuwa kwa Gidioni, na jambo hilo lilimuumiza sana.
Nahisi atawewe unajambo ambalo kama Bwana angejifunua leo ungemuuliza, yawezekana lina kuumiza sana, tena kwa namna ulivyozipokea habari za Yesu, hukudhani kama jambo hilo lingeendelea kuwa gumu kiasi hicho, embu jifunze hapa namna Roho Mtakatifu alivyoamua kuingilia kwa Gidio ilikukuvusha na wewe;

(Naamini tuko pamoja, Kama ndio sema ndio, Kama sio Roho mtakatifu arudishe mawazo yako hapa ili upokee alichokusudia)
Nachotaka tujifunze ni namna Mungu alijifunua kupitia Gidioni ili kuliokoa taifa la Israel; na kitu cha msingi ndani yangu natamani ujue namna utukufu ule ulioshuka kwa Gidioni uliweza kuwa sehemu ya Gidioni miaka mingi kupitia nguvu ya kuoa Sadaka, sema tena nguvu ya Sadaka).
Gidioni alipata kibali mbele za Mungu, lakini shida kwake si kama alikuwa anataka kibali ila anachotaka ni uhakika wa taifa lake kuwa salama, na Mungu asingeweza kumtumia bila kibali, Gidioni akaamuwa kutafuta uhakika,uthibitisho wa kuwa Mungu atamtumia yeye na kuhakikisha wanatoka kwenye eneo linalo wasumbua.

Nisikie vizuri hapa, Si Malaika alimuomba Gidion sadaka, lakini Gidion alipoona Malaika amejifunua mbele yake alimuomba Malaika asiondoke mpaka amtolee sadaka,

 Malaika alifurahia na kuahidi kuisubili, ni msukumo wa ndani aliokuwa nao Gidion, tena ni siri ambayo Gidion alikuwa anajua, lengo la Gidioni ni kujiunganisha na Mungu kwa njia ya Sadaka, ili kuruhusu uthibitisho wa Mambo ya kimungu, pia ili kuruhusu kufuatiliwa na nguvu za Mungu. Biblia inadhihirisha nguvu iliyomo kwenye sadaka,

Tutaendelea Sehemu ya pili ya somo hili.
..... Mambo yakuzingatia utoapo sadaka"
@Huduma Ya Gombo La Chuo (Daniel Mwaitenga)
Share:
Designed and Developed by Joel Elphas 0757 755 228 or 0655 755 228 © HUDUMA YA GOMBO LA CHUO ...Ukawaambie maneno yangu. Ezekiel 3:4 | ronangelo | NewBloggerThemes.com