Matendo ya Mitume 7: 18 “Hata
mfalme mwingine akainuka juu ya misri, asiye mfahamu Yusufu.”
Tazama pamoja na mimi maneno haya; (MFALME
MWINGINE), (MISRI) na (ASIYE MFAHAMU YUSUFU).
Kuna
maneno ya msingi sana tuyatazama katika tafakari hili kupitia Matendo ya mitume
7:18, ni yamuhimu wewe kuyafahamu ya kupeleke kwenye lengo la tafakari letu,
Kwanini imeandikwa “mfalme mwingine”
…..(Misri)……. “asiye mfahamu Yusufu”
Ndugu
wa Yusufu (familia ya Yakobo) wakiwa, utumwani(misri) waliishi katika mazingira
mazuri sana, kwasababu Yusufu alikuwa kwenye utawala wa juu, pamoja nakuwa ni
utumwani MUNGU alimpa kibali na akapewa wadhifa mkubwa sana.
Nielewe
hivi, mfano; hata ukifanya kazi benki wakati huna elimu/ujuzi stahiki, ni sawa
na mtu anayeishi utumwani, ni muhimu sana ujue yawezekana si kosa mana kwako ni
muujiza, ila fanya maandalizi mana kuna siku utawala utabadilika. Au, yawezekana
kuna kazi umepata, kama muujiza tu, au kwasababu wewe ni mzuri tu, au kwasababu
ya umaarufu wa watu Fulani n.k; ila ukweli wa dhati kabisa elimu ya/ujuzi wa
kazi hiyo hauna……..jiandae…..tena jiandae.
Kuna
mabadiliko mbele sijui umejiandaaje, hata kama umeokoka wewe fanya maandalizi.
Muujiza
huwa unakikomo (umejiandaaje baada ya muujiza huo kuisha), anakuja mtawala
ambaye hana hobi ya kutazama uzuri wako kazini, au mtawala ambaye hajuani na
huyo mtu maarufu aliyekufanya ukae hapo; wakati huo huyo mtu maarufu hayupo
tena duniani.
Inawezekana
haupo mahali sahihi lakini maisha
yanaenda vizuri sana, sababu mtawala wa eneo hili amempa wadhifa mkubwa ndugu
yako na ndugu yako akakufanya uishi maisha mazuri hapo. Lakini umejiaandaaje
endapo ndugu yako akafa au akatolewa hapo na akainuka mfalme mwingine asiye
mfahamu Yusufu( ndugu yako).
Mfano:
huna elimu ya kufanya kazi benki, lakini unafanya kazi benki, kwasababu meneja
aliopo anafahamiana na babayako, je, siku anakuja meneja mwingine “asiye
mfahamu baba yako”, umejiaandaaje?
(ukweli pamoja nakuwa umetoa ushuhuda kanisani
kuwa Bwana ametenda kwa wewe kukaa nafasi ambayo kiuhalisia huna ujuzinayo, na
sababu iliyokuweka hapo yawezekana ni kama muujiza au ni kibali na kujulikana
kwake baba yako; …umejiaandaaje mpendwa?)
Wana
wa Yakobo walipata wakati mgumu sana, wakati Yakobo amekufa, na Yusufu amekufa;
mbaya zaidi ameinuka mfalme mwingine
asiye mfahamu Yusufu; maisha yao yalibadilika kabisa, historia yao
ilibadilika kabisa, kosa ni kwamba walifikiri kuwa milele Yusufu ataishi au
milele Yule aliyempa yusufu nafasi ataishi.
Haijarishi
umeokoka kiasi gani swala la wewe kuwa namaandalizi ya mabadiliko kwa mambo ya
mbele na mabadiliko ya kiutawala ni muhimu sana. Haijarishi ni Mungu kakuweka
hapo, swala la wewe kumuuliza Mungu mambo ya mbele na kumsihi kukuandaa
kuyakabili na kuyashinda mabadiliko ni muhimu sana.
Ukipewa
nafasi kwasababu Fulani ambayo kimsingi hukustahili, imepatikana kiujanja
ujanja tu, au kwaneema tu au muujiza
ambao yawezekana lengo la Mungu wakati huo ni kukustili kwa wakati
wakitambo kifupi tu, basi jifunze sana kujiandaa kwaajili ya kuimiliki na fasi
hiyo kwa haki na ujuzi stahiki; ili kuyakabili mabadiliko yoyote ambayo kamwe
hayata angalia umaalufu wa babayako,
ndugu zako, au uzuri wako.
@Daniel Mwaitenga.