UMEKUWA NA BIDII SANA KATIKA KUMTAFUTA MUNGU,LAKINI MAMBO BADO NI MAGUMU NA UKITAZAMA WASIO MCHA BWANA NDIO KWANZA WANAZIDI KUFANIKIWA
NINI
LAKUFANYA?
Mathayo 11: 28-29 “Njoni
kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami NITAWAPUMZISHA,
jitieni nira yangu MJIFUNZE kwangu, kwakuwa mimi nimpole na mnyenyekevu wa
moyo, nanyi mtapata RAHA NAFSINI mwenu.”
Ukiona
mtu amekaa sana kanisani au katika wokovu kwa miaka mingi sana alafu haoni
mafanikio, uwe na uwakika kuwa ni rahisi sana mtu huyo kutafuta mafanikio nje
ya kanisa/nje ya wokovu.
Ukiona
mtu ametumikia sana mashetani alafu hapati mafanikio na kama anapata kwa muda
mrefu amekuwa hapati amani kupitia mafanikio hayo,uwe na uwakika atakuja
kanisani kutafuta mafanikio kama hana,na kama anayo ila hana amani nayo atakuja
katika wokovu kuyatafuta mafanikio yenye uhuru na amani.
Nielewe vuzuri hapa; nataka ujue
kila mtu anatafuta mafanikio, wala sio dhambi; kosa ni moja tu,kufikiri kuokoka
ili uafanikiwe tu; nakushindwa kujua kuwa wokovu ni mafanikio na ni zaidi ya
kufiri kufanikiwa(kustahimili kuwa na kristo hata nyakati ngumu kimaisha).
Japokuwa kunakipindi unaweza kufikiri kuwa hakuna maana ya wokovu kama UMEOKOLEWA
alafu hunatofauti na ALIYETEKWA,lakini
si kila anaeshi kama mateka ndani ya wokovu ndio mwisho wa ajenda ya Mungu
kwakwe.
NOTE:
Nataka ujue kuwa, moja ya mambo ambayo Mungu anayathamini ni mafanikio ya watu wake, ambayo chanzo
chake ni amani, furaha na haki na
mjumuisho wa mambo haya,Yesu aliuita raha
nafsini mwako, hakuna raha kwenye nafsi kama hakuna mafanikio hata kidogo;
Nimuhimu pia ujue kuna utofauti wa kupumzishwa
na kupewa raha nafsini mwako.
Sasa, nataka nikwambie Mungu hawezi kukupajibu
lolote katika hali ngumu hiyo bila yeye kukufundisha
kitu katika ugumu huo na njia yakutoka hapo.Lakini ni mihimu sana ujue upande
wa Mungu mafaniko yanapatikana na yanakanuni zake, na shetani nae anatoa
mafanikio yenye kanuni zake, ambazo kwa wakati huo wanjaa na ugumu huwezi kuona
kama zina maana ila yeye anajua kuwa; lakini hata sikumoja shetani hafurahii
kufanikiwa kwa mwenye haki,hivyo ukifanikiwa atakupinga sana.
Ukipita kwenye
wakati mgumu kama huo na maswali kama hayo, unatamani kama Yesu angesema; kachukue
pesa sehemu Fulani, au nenda ofisi Fulani watakupa ajira ili tatizo liishe; Ninao
ujasiri wa kukutia moyo ktk Jina la Yesu kristo kama utakubali kujifunza.
NINI
LAKUFANYA:
##
Ayubu 21:7, 9 “Mbona waovu wanaishi,na
kuwa wazee, naam, nakuongezeka (kustawi) nakuwa na nguvu? Nyumba zao zi salama
pasina hofu, wala fimbo ya Mungu haiwapigi?”
1. Usichanganyikiwe na mafanikio ya
waovu,ila USIRIDHIKE kwa kukosa mafanikio ukiwa ndani ya kristo, namaanisha
hivi, kama utajaribu kuchanganyikiwa na mafanikio ya waovu ni rahisi sana wewe
kukubalina na njia zao ili kupata mafanikio,sababu wewe shida yako ni mafanikio
tu;lakini lazima ujue hatima ya kustawi kwa waovu ni wapi. (Zaburi 92:7 “wasio
haki wakichipuka kama majani, na wote watendao maovu wakistawi, ni kwa sudi
waangamizwe milele).
##
Habakuki 1:2-4 “Ee Bwana nilie hata lini,wewe usitake kusikia?Nakulilia kwa
sababu ya udhalimu ila hutaki kuokoa. …. kwasababu hiyo sheria imelegea,wala
hukumu haipatikani; kwa maana watu wabaya huwazunguka wenye haki,kwasababu hiyo
hukumu ikipatikana imepotoka.
2.
Jitahidi sana hali hiyo ngumu isivunje mahusino yako na Mungu,Bado Mapepo
yanayo pigana nawe yakikuona yaseme YESU TUNAMJUA NA WEWE TUNAKUJUA.
Penda
kuwa mtu wakuzungumza na Mungu kila wakati (MAOMBI), mana katika hali hiyo ni
rahisi sana kumsikia Mungu wakati wowote atakao jifunua kwao ili kusema nawewe.
Mwanzo
12:10-20; 26:1-2.
3.
Usilazimishe kupita njia walizo pita wengine, wakati umejaribu na zimegoma,
hata kama nao walipitia hali hiyohiyo na niwakristo wazuri tu, ni muhimu
umsikilize Mungu.
Mwanzo
26:12-14
Sikia
Ibrahimu alipoona njaa akakimbilia misri, lakini wakati wa Isaka njaa ilipokuwa
kali, alitaka kwenda misri kama Ibrahimu alivyofanya lakini Mungu akamwambia usiende ila mahali hapohapo pakame
wewe panda na utavuna,Bwana akabariki mashamba na mifugo yake na akamtajirisha.
4.
Ufanye wakati huo kwako kuwa rafiki sana na mafundisho ya Neno la Mungu kwa
undani zaidi, mana Yesu anasema JIFUNZENI KWANGU NANYI MTAPATA RAHA NAFSINI
mwenu.kubali kujifunza kwa yesu hicho unacho kihitaji wakati huo kupitia
mafundisho utajua utofauti wa yeye kukupumzisha na kukupa rahanafsini mwako.:
5.
Tazama MBINU unazo zitumia kwa wakati huo wote na sababu ya kutokufanikiwa
huko. mfano MOJA, yawezekana unalalamika tu kwa Mungu lakini huna muda
kumsikiliza Mungu ilikujua kunanini ndani yako na majira yake, PILI, yawezekana
unatalanta lakini huzifanyii kazi, TATU, yawezekana BIDII yako ya kufanya kazi
na ujuzi au ubunifu wa kazi hiyo umevikosa. ni muhimu sana kujua KANUNI za
KIUCHU kutoka kwenye mfumo wa Mbinguni.tunae roho wa ubunifu sawa na kutoka
31:1-5.
MAMBO
YA MUHIMU UNAYOWEZA KUJIFUNZA KUPITIA HABAKUKI ALIPOPITA KWENYE KIPINDI KAMA
HIKI:
Moja, hata kama umepita pagumu sana
na umetumia juhudi zako bila mafanikio; tulia chini sasa kwenye nafasi
yako,katika utulivu wa kusoma neon na maombi ya utulivu sana,usikie nini Mungu
atazungumza na wewe.
Mbili, amini jambo hili;haijarishi nini
unapitia au kuna ugumu gani kako, ume umbwa kwa kusudi na ndani yako kuna NJOZI
itakayo kutimiza kusudi hilo( iandike vizuri)
Tatu,usiwe na haraka sana Majira yana
wadia si muda mrefu na wakati huo utafurahi.
Mwisho, Habakuki tangu hapo alianza
kumuogopa Bwana mana alijua kuwa upompango mzuri juu yake, akasema kumbe fufua
hata kazi yako iliyokufa katikati ya miaka, na hataka kama ntakosea kumbuka
rehema.(sifa za Bwana na kufufuliwa kwa vitu vilivyo kufa au vusivyo zaa ndani
yako).Amen.
@Mwaitenga
D.