LENGO LA MUNGU KUTAKA UJUE
UMUHIMU WAKUTAMBUA NAFASI YAKO YAKIROHO KATIKA KAZI/AJIRA YAKO
Utangulizi:
Tuombe:
Ili:-
Moja, Ikusaidie kujua kusudi la Mungu kukuweka hapo, na mbinu za kutumia wakati wa kutimiza kusudi hilo zaidi katika upinzani utakao kutana nao.
Esta 4:14 “Kwa maana wewe
ukinyamaza kabisa wakati huu,ndipo
kutakapowatokea wayahudi msaada na
wokovu kwanjia nyingine;ila wewe utaangamia pamoja na mlango wote wa baba
yako;walakini ni nani ajuaye kama wewe
hukuujia ufalme kwaajili ya wakati kama huu?”
U- Malikia wa
Esta haukuwa ni ajira au umaarufu tu, ila ndani yake ulibeba kusudi la Mungu,
kushindwa kuyajua hayo mapena katika nafasi ya kiroho kulimgarimu Esta wakati
wa kulitimiza kusudi, ,Hamani alikuwa ni mpinzani wa Mordekai na sio Esta, bali
upinzani wa Esta ilikuwa ni Sheria na
taratibu za Ufalme.
unapotaka
kutimiza kusudi la Mungu kupitia kazi yako na upinzani ni mkubwa si lazima
utumie taratibu za kazi yako ila nafasi yako ya kiroho ndio itahusika hapo kwa
kutumia mbinu za ulimwengu war oho kuzinyamazisha sheria za kimwili.Esta baadae
sana alipoyajua haya Roho Mtakatifu anayokufundisha sas, ndi akajua kuwa Maombi
na Mfungo vitumike, wakati mwanzo alitaka kutumia sheria na taratibu za kazi.
Pili, ni kukusaidia nafasi yako ya kiroho kuitawala
na kuiongoza kazi yako na sio kazi yako kuongoza nafasi yako ya kiroho.
Mwanzo 3:9-12
“……Bwana Mungu akamwita Adamu,akamwambia, uko wapi?...”Ukijua nafasi
yako huta ziruhusu sababu zilizo nje ya sheria na taratibu za aliyekupa nafasi
hiyo,zikutoe kwenye nafasi yako.
Tatu, kukusaidi kuipenda kazi yako nakufanikiwa
katika hiyo,pasipo jarisha kwa wakati huo wengine wanaichukia au wanaipena,
wamefanikiwa hapo au hawajapata mafanikio kulingana na mazingira yanayo
kuzunguka.
Unajua unaweza
ukaitumikia jamii vizuri sana tena wakakupenda sana, lakini Mungu asipate faida
yoyote katika utumishi wako kwa jamii; Fikiri kama Esta aliitumikia jamii
vizuri alafu angeheshimu sheria na taratibu za kazi yake ili jamii impende, na
kusudi la Mungu lishindwe kutimia kupitiayeye wakati Mungu ametumia gharama
nyingi kumuandaa nini kingetokea?
Nne, ni kujua kuwa kama ni Mungu amekupa kazi hiyo,
basi anatake kufanya kazi pamoja nawewe Tazama
Rumi 8: 28 “… katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao….,wale
walioitwa kwa kusudi lake…”
Mwisho, kama haupo kazini ujaya jua haya, ipo
neema ya Mungu kubwa kukusaidia kurudi kwenye nafasi yako, tena, kupata faida
za kuijua nafasi na kuitumikia. Baada ya Musa kukaa kwenye nafasi yake Mungu
akaanza kuzungumza nae, Musa akwa na uhuru pia wa kumuuliza maswal, vivyo hivyo
Habakuki na wengine wengi
Kutoka 3:2 – 4
“…..;akatazama, na kumbe! kile kijiti
kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea. Musa akasema, “nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki
hakiteketei.”Bwana alipoona yakwa amegeuka
ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kilekijiti,….”
Inawezekana wewe
ni Mwalimu, Daktari, askari jeshi/polisi, mkulima, mfanyabiashara n.k, lakini
sijui kama umewahi kupata muda wakutamani kujua kazi unayofanya au maisha unayoishi kwa ujumla yana mahusiano gani na nafasi ya kiroho ambayo Mungu amekuumbia na kukuweka kwenye
kazi hiyo ili upitishe kitu cha ufalme wake.Mana nina uwakika kuwa kuulipata
muda wa kumuomba Mungu sana ili upate kazi, na yawezekana unatekeleza majukumu
yakazini vizuri sana tena kwa bidii na kwa kufuata sheria za kazi vizuri.
Lakini kunakitu
kikubwa sana ndani ya hiyo kazi ambacho kama ujakaa kwenye nafasi yako, unaweza
ukafanya kazi vizuri na kutumikia jamii ila usiwe na faida yoyote katika ufalme
wa Mungu mbali na kuwa ulimwomba Mungu na ndiye kakupa kazi hiyo, si wakristo
wengi huwa wanakihitaji hicho hasa wakisha pata kazi.(mfano:Esta alikuwa
malikia, ila Biblia inaonesha sura ya 4 kuwa katika ulimwengu wa roho umalikia
wake ulibeba kusudi la Mungu ambalo yeye alipa shida sana kuelewa mpaka alipo
ijua nafasi yake na kuanza kuitumia….) Na ndio maana wengi wanafikiri kutimiza
kusudi la Mungu ni jambo la kazi za kanisani tu,kama kuwa mihubiri.
Embu tazama siri hii kubwa ya ajabu sana
soma Daniel 4:34-36, na ndio maana 4:1 aliamua kutangaza kwa kila kabila,lugha jamaa na taifa.
atakama kazi yako imesitawi sana usipojua nafasi yako katika ulimwengu wa roho ni rahisi sana kumsahau Mungu, kuongoza vile ufikilivyo wewe, Kumbe ni muhimu ujue mbingu na zikutawale katika miliki hiyo ni Mungu anamiliki.
Sasa fuatana na mimi hapa:
Daniel 4:20-22
“ …… ni wewe, ee mfalme, uliyekuwa na kupata nguvu; mana ukuu wako
umekuwa na kufika mbinguni, na mamlaka yako yamefika mpaka mwisho wa dunia.”
(huo ni ustawi wa ufalme(kazi yake)
Daniel 4:25-26…..hata utakapojua yakuwa aliyejuu
ndiye anae miliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa yeye amtakayeawaye
yote.na kwakuwa waliamuru kuiacha kisiki cha shina lake, ufalme wako utakuwa
imara kwako, baada ya wewe kujua yakuwa mbingu ndizo zinazo tawala.
(huu ni upungufu wake pamija na kustawi kwake)
Ni siri kubwa sana za ajabu sana,ambazo Mungu anamfunulia
mtumishi wake Mfalme Nebukadreza; Kwamba ni kweli nafasi yake ya kazi imekuwa
sana yani ufalme wake katika kutawala na kumiliki, lakini kuna kitu kimoja kimepungua
na hicho ndicho Mungu anakitaka kwake,
Hajajua bado ni nani anaemiliki katika ufalme wa wanadamu,
na nini kinacho tawala.
kwa lugha nyepesi mfalme hajajua nafasi yake yakiroho ambayo ndiyo inayo mtambulisha nini na nani anamiliki na kutawala.
Embu tazama baada ya adhabu aliyopewa yenye lengo la kumfanya mfalme ajue nafasi ya Mungu;
soma Daniel 4:34-36, na ndio maana 4:1 aliamua kutangaza kwa kila kabila,lugha jamaa na taifa.
atakama kazi yako imesitawi sana usipojua nafasi yako katika ulimwengu wa roho ni rahisi sana kumsahau Mungu, kuongoza vile ufikilivyo wewe, Kumbe ni muhimu ujue mbingu na zikutawale katika miliki hiyo ni Mungu anamiliki.
Sasa fuatana na mimi hapa:
1. Inawezekana katika eneo/mazingira ulipo au kazi
hiyohiyo unayofanya ikawa ni kazi sahihi katika mazingira sahihi na muda sahihi
lakini ukashindwa kutimiza kusudi la Mungu kwa kushindwa kujua nafasi yako au
kutokuwa kwenye nafasi katika ulimwengu wa roho.
Mwanzo 3:9-12
“……Bwana Mungu akamwita
Adamu,akamwambia, uko wapi?...”
Kwa lugha nyepesi,
Adamu hakuwa kwenye nafasi yake,
ambayo Mungu anatakiwa kumkuta,au ambayo alimuweka na huwa wanakutana katika
hiyo. Na Adamu anajua nafasi yake
lakini kwa wakati ule anakili hakuwa kwenye nafasi yake kwa sababu Fulani. , ila cha kushangaza
alikuwepo mazingira yale yale ya bustanini kwa muda ule; ndipo utapata picha
kuwa ni nafasi ya kiroho. (jipya hapa…kumbe, kazi ya shetani ni kukutoa
kwenye nafasi yako kwa kutumia
mageuzi ya sheria na sababu zilizofanya ukawekwa kwenye nafasi hiyo, na ili
utoke kwenye nafasi yako inategeme sana mambo mawili (2), moja kujua nafasi yako, pili
kushikilia maelekezo na sheria ulizopewa na aliyekupa nafasi mana ndizo zitakazo
kufanya usitolewe kwenye nafasi hiyo.Nimuhimu pia,ujue kuwa zipo sababu nyingi
za kukutoa kwenye nafasi yako.
Kitendo cha kushindwa
kujua nafasi yako au kutokuwa kwenye nafasi yako ni kuruhusu kuishi nje ya mipango
na kusudi la Mungu. Hata kama upo eneo hilohilo kama ilivyo kuwa kwa Adamu,
tena unaweza hata kuondolewa katika
mazingira sahihi kama adhabu.
2. Inawezekana
unatimiza majukumu yako vizurikazini, kwa kfuata utaratibu sawa na sheria za kazi
zinavyo kutaka, bosi/mwajiri wako anafurahi na watu wanafurahi lakini katika
ufalme wa Mungu usiwe umepata faida yoyote, kwasababu tu hujatambua au haupo
kwenye “nafasi yako kiroho” katika kazi hiyohiyo na kushindwa kujua nini Mungu
anataka kupitia kazi hiyo ukipitishe ili kijenge ufalme kwake , japo sawa unawatumikia
watu vizuri.
Tazama Mordekai
na Esta;
Esta 4:14 “Kwa maana wewe
ukinyamaza kabisa wakati huu,ndipo
kutakapowatokea wayahudi msaada na
wokovu kwanjia nyingine;ila wewe utaangamia pamoja na mlango wote wa baba
yako;walakini ni nani ajuaye kama wewe
hukuujia ufalme kwaajili ya wakati kama huu?”
Nachotaka
ujifunze hapa ni kwamba; Esta kuwa malikia si kwasababu alikuwa mzuri sana japo
ni moja ya kigezo kilicho tumika,tena kama ni msomaji mzuri wa Biblia pamoja na
uzuri wa Esta, bado hakustahili kuwa malikia mana kuna vigezo ambavyo hakuwanavyo,na
hivyo hakutakiwa kuwa malikia. mfano utaifa,kumbuka
alikuwa utumwani ndio maana alikatazwa na Mordekai asitaje kabila wala jamaa
yake.(swala la utaifa ni muhimu
kuliko uzuri,mana ni rahisi mtu wa taifa jingine kumdhuru mfalme au kuruhusu
maadui wa upande wake) Lakini kusudi la Mungu lilimuhitaji Esta awe malikia ili
Mungu apitishe uponyaji wa taifa lake, moja ya sifa kuu, nikuwa, alitakiwa kuwa na uzuri wa umbo
na uso. Kwahiyo utakubaliana na mimi kuwa ilimlazimu Mungu kumuumba Esta katika
uzuri ule nakufanya mazingira ambayo yatazaa matokeo ya kusudi la Mungu kutimia.
Haijalishi alipitia ugumu gani kama uyatima aliokuwa nao ila kuna mchakato
uliokuwa ukiendelea katika ulimwengu wa roho na ulitimia.
Kosa la Esta:
Esta alikuwa
Malikia ambaye hakujua NAFASI yake katika ulimwengu wa roho ila alijua katika mwili
tu, ukiniuliza kwanini, ntakwambia alifuata sheria zote na taratibu kama
impasavyo kwa kuhudumia jamii na jamaa yake vizuri.Kumbuka kuwa pale Esta
alikuwa mazingira sahihi, na wakati ule ulikuwa sahihi kwa Esta
kuanza swala la ukombozi ambalo ndio kusudi
sahihi,ila hakujua nafasi yake,sijui
uemenielewa hapo.Pili yeye alijua kuwa anatakiwa sana kumtunza mjomba wake
Mordekai” ndio maana tatizo lilipotokea la wao kutaka kuuwawa hakujua nafasi yake kabisa ntakwambia kwanini.
Alicho kifanya ni kumtuliza Mordekai kwa
kumpelekea mavazi; akifikiri
amemaliza mana nafasi hiyo kimwili alikuwa anaijua na alikuwa sahihi kabisa,
lakini hakujua katika ulimwengu wa roho.
Sikia sasa,
moja ya kazi ya
Mordekai ilikuwa ni kumtengenezea Esta mazingira ya kuketi katika nafasi ile
kimwili na kiroho, lakini Kosa la
mordekai, hakumuandalia Esta mazingira ya kuijua nafasi yake katika nafasi
ya ufalme kwa picha ya rohoni, ndio maana ilimsumbua sana Esta, si kwamba
alikusudia kujibizana na Mordekai kwa muda mrefu, hapana yeye alikuwa
anamuelewesha kufuatana na katiba au sheria, mpaka wakati ufahamu wake
umefunguliwa ndipo akajua nafasi yake na akaanza kutumia mbinu za kiroho yani
si maombi tu,bali kwa gia ya mfungo ,wauuh!
Esta mwishoni alipojua nafasi yake katika ulimwengu wa roho alisema mkafunge na
kuomba siku tatu (3), nami ntafunga na watu wangu na nitaingia kwamfalme kinyume
cha sheria.
Nataka ujue kuwa
inawezekana kazi unayofanya ni sahihi,na upo mazingira sahihi na wakati sahihi,
tena nimpango wa Mungu wewe kutimiza kusudi lake kupitia kazi hiyo.Lakini ni lazima ujue kuwa si elimu tu
imekupa nafasi hiyo,japo nikigezo kimojawapo, lakini kuna mkono wa Bwana,hivyo
nilazima pia ujue nafasi yako katika ulimwengu wa roho, na ukijua hayo utatimiza
kazi hiyo kwa taratibu na sheria za kazi yako,na inapofikia kupitisha kusudi la
Mungu kama kuna kitu kinazuia basi si razima uendane na sheria na taratibu za
kibinadamu zilizowekwa katika ofisi yako, hasa mazingira yale yanayonyima
kusudi na mpango wa Mungu kufanya kazi. (mfano; Esta 4:16…Esta akasema
mkaombe…nitaenda kwa mfalme kinyume cha taratibu).Mana yake asingejua hilo,
u-malikia wake usingekuwa na faida yoyote kwa Mungu.
3. Ni rahisi sana Mungu kujifunua kwako; lakini nivigumu sana yeye
kujitambulisha kwako kuwa yeye ni nani katika hilo unalofanya au analotaka
ufanye, na yeye atakutambulisha kuwa ni nani kwa jamii unayo ihudumi; pia ni
vigumu kuwa namazungumzo nawewe, hata kukusihi
yakupasayo kufanya kama kutubu kwa kutambua uwepo wake kwako mpaka
utakapo kaa kwenye nafasi yako kiroho katika kazi unayofanya, katika maeneo
ambayo unaweza kuyaona kuwa niyakawaida sana. Kwasababu unapokuwa katika nafasi
yako ni rahisi kuyaona maono yani kuuana kujifunu kwake katika picha ya kiroho
na kumuelewa.
Kutoka 3:2 – 4 “…..;akatazama, na kumbe! kile kijiti
kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea. Musa akasema, “nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki
hakiteketei.”Bwana alipoona yakwa amegeuka
ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kilekijiti,….”
Umewahi
kujiuliza kwanini Musa alipo kuwa mlima wa Mungu (Horebu) Mungu akuanza
kuzungumza nae mpaka alipo alipogeuka
(katika ulimwengu wa roho)., ndio maana alisema niyaone maono lakini mwanza pamoja
nakuwa aliona kijiti kinawaka na hakiteketei aliona kimwili tu, cha ajabu
Biblia inasema Mungu alioona amegeuka
ndipo alianza kusema nae, yapo mengi utajifunza pindi utakapo jua kukaa
kwenye nafasi yako kiriho katika kazi unayo iona ipo kimwili, moja(1), ukijua nafasi ni rahisi kutubu soma
hapo kwa Musa,Mungu akamwambia mahali hapa ni patakatifu maana yake Musa
alikuwa hajui wakati huo na kuambia
ajitakase pale; pili (2), nirahisi
kuanza kuwa na mazungumzo na Mungu; Tatu(3), ni rahisi Mungu kusema yeye ninani hapo katika kazi yako;
nne(4), ni rahisi wewe kumuuliza Mungu kwanini amekuweka hapo
(hata ukitaka kujifanya mbabe na kukataa hiyo kazi usikatae kabala ya kujua
nafasi yako, ukijua nafasi yako ni rahisi kujua nafasi ya Mungu hapo na
kumuhoji maswali.)ni mbaya sana kukataa kazi sehemu Fulani kama hujajua nafasi
yako hapo na ya Mungu kwako kuwa hapo, tena itakgharimu.
4. Njia mbili zitakazo kusaidia kuijua nafasi yako
au kurudi kwenye nafasi yako
Moja; Neema ya Mungu ikusaidie Ugeuke (Kutoka 3:3 na Habakuki 2:1)
Unajua ni vigumu
sana kujua uwamuzi alio uchukua Musa kusema natageuka, au Habakuki kusema name
nitasimama kwenye zamu yangu, ni uwezo wa kufanya maamuzi na kuchukuwa hatua
kwa kuitumia ile neema iliyo juu yako. Ndipo damu ya mwana kondoo inakutakasa
na kukupa fulsa ya kumuona Mungu.
Pili; kupitia mafundisho (neno la Mungu)kupitia watumishi wake kwa Roho mtakatifu(Esta
4:1-17).
Unaweza
kujifunza pamoja nakuwa palikuwa na ugumu mkubwa sana, ila nguvu ya Mungu ndani
ya Mordekai ilikuwa inamlazimisha mordekai kumpa elimu Esta ili ajue na fasi
yake, japo kosa ni la Mordekai kama mtumishi alimuandaa Esta katika nafasi ya
mwilini na kujisahau eneo la rohoni.Ila swala ni kujitahidi sana moja watumishi
wa Mungu kufundisha na kuandaa watoto katika hali zote, wazazi pia.AMEN
na Daniel Mwaitenga.
@0768815059/0714373259