KWANINI ASILIMIA KUBWA YA WATUMISHI WA MUNGU (WAKRISTO) WANAPOANZA KAZI HASA ZA MAOFISINI AU WANAPOHAMIA MAZINGIRA MAPYA MAHUSIANO YAO NA MUNGU YANAVUNJIKA?
Tafakari (somo) langu lipo katika mfumo wa swali, na Lengo la somo
hili ni kuwasaidia watu ambao katika maisha yao wanakutana na mazingira kama
haya:-
1. Watu ambao
wanadhohofika taratibu au wamekufa kabisa kiroho, mara tu, walipoingia na kuanza kufanya kazi katika
ofisi fulani au kuishi mazingira fulani, hasa kwa kuiga tabia za wenyeji wa
ofisi hiyo/mazingira hayo kwa kujua au kutokujua;
Mfano 1. Rafiki zangu wengi ni waalimu na wapo katika
mazingira ambayo ni mapya ki-maisha na ki-kazi, napozungumza nao, wengi
wanasema mahusiano yao na Mungu si mazuri, bidii ya kutumika imeisha, nguvu ya
kuomba haipo, na mambo waliyokuwa wanadhani hawatayafanya au walikuwa
wanayachukia yasiyo ya haki mbele za Mungu, nawao wameiga na wanayafanya sawa
na wenyeji wao.
Mfano 2. watu ambao
wanafanya kazi katika maofisi Fulani, kwamba toka walipoingia kuanza kazi
taratibu hatua zao za kusonga mbele kiroho zina fifia, sababu kubwa ni namna
ofisi zao zinavyo watengeneza, Maisha yao ya kazi yamefunga maisha yao ya
kiroho, fahamu zao hazifikiri habari za Mungu tena.
2. Watu ambao
wamejiingiza kwenye tabia mbaya kama uzinzi na maovu mengine, na asili ya maovu
hayo chanzo chake ni kutokana na kuiga tabia za ofisini kwa mabosi wao au
wafanya kazi wenyeji walio wakuta mahali pale.
3. Kuumizwa mara kwa
mara katika ofisi zao, na mabosi wao au wafanyakazi wenzao ambao ni wenyeji,
4. Wanafukuzwa kazi kila
mahali wanapo ingia, ukipata kazi haukai zaidi ya mwaka, unafukuzwa,
Mfano:
Umewahi kujiuliza kwanini Daniel alipoingia Chuoni hadi kufuzu
kukaa katika utumishi wa nyumba ya mfalme kwa mara ya kwanza tu, alikataa kula
chakula na kunywa divai ya Mfalme kwamba vitamnajisi?(Daniel 1:1-8)
Jibu ni kwamba
“alitahadharisha NAFSI yake ili kuepuka kujiingiza kwenye MAAGANO ya miungu
iliyokuwa katika ofisi ile na mazingira yale kwa lengo la kukwepa kujiingiza
katika MITEGO ya kumilikiwa na miungu migeni.
Hilo ndio kosa kubwa
sana, wengi hawajajua kushughulikia maeneo au ofisi mpya katika ulimwengu wa
roho ili kuhakikisha Mungu anafanya kazi pamoja nao maeneo hayo na kuimarisha
mahusiano mazuri na Mungu.
SOMO HILI LINA KUHUSU
WEWE KWAAJILI YAKO AU KWAAJILI YA NDUGU/ RAFIKI YAKO.
UTANGULIZI:
SOMA NAMI:
(Kumbukumbu la Torati
7:1) Bwana, Mungu wako, atakapokutia katika nchi uendeayo kuimiliki, …………..
(Kutoka 34:12) Ujihadhari nafsi yako, usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi ile unayoiendea lisiwe mtego katikati yako………………
(Kutoka 23:33) kwasababu ukiitumikia miungu yao, jambo hili
halikosi litakuwa ni tanzi kwako.” ……………
(Kutoka 34:13)Bali
utabomoa madhabahu zao…….
(kutoka 23:25-26) nanyi
mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, nae
atakibarikia chakula chako, na maji yako.Nami nitakuondolea magonjwa kati
yako.Hapatakuwa na wenye kuharibi mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako;na
hesabu ya siku zako nita itimiliza.
Kwanza tafakari vifungu hivyo hapo juu, wewe
binafsi; Kisha Fuatilia somo hili
wiki ijayo kama tafakari la wiki ijayo litakusaidi, mana tutatazama sababu na
njia za kutatua…………………Amen!!
……Itaendelea
@Daniel Mwaitenga.