... ukawaambie maneno yangu. Ezekiel 3:4




SHALOMU TANZANIA!! HUDUMA YA GOMBO LA CHUO INAWATAKIA UCHAGUZI MWEMA WATANZANIA WOTE.

TAFAKARI NASI WIKI HILI LA UCHAGUZI. 

NGUVU YA MAOMBI YAKO KWENYE KURA YAKO.

Nenda kapige kura mtanzania kuna maana sana kibiblia; Tazama hapa


 MATENDO YA MITUME1:23-26

Wakaweka wawili, Yusufu,aitwae Barsaba, aliye kuwa na jina la pili Yusto, na Mathiya, KISHA WAKAOMBA wakasema, “wewe BWANA, UJUAYE MIOYO YA WATU WOTE TUONYESHE NI NANI ULIYE MCHAGUA KATIKA HAWA WAWILI, ashike mahali katika huduma hii na utume huu, alioukosa Yuda, aende zake mahali pake mwenyewe”.WAKAPIGIA KURA; KURA IKAMWANGUKIA MATHIYA;nae akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na moja.

YOSHUA 3:5 Yoshua akawaambia watu, “jitakaseni, maana kesho Bwana atatenda mambo ya ajabu kati yenu.”

Leo natamani upate muda wa kutafakari,


*Moja, kwanini hawa mitume waliomba na kisha wakapiga kura, hatimaye aliye angukiwa na kura akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na moja.(kuna nguvu kwenye kura itokanayo na mwongozo wa Mungu mwenyewe.)

*Pili, kulikuwa na umuhimu gani wa taifa la Israel kujitakasa kwanza ndipo Bwana atende jambo la ajabu ktk muda huo.(ukitaka mambo ya ajabu yatimilike,kaa ktk hali ya utakaso yani mruhusu Mungu kufanya alicho kusudia,)

HAYA MAMBO YATAKUSAIDIA KUJUA, UMUHIMU WAKUOMBEA UCHHAGUZI, MAANA YA KUPIGA KUURA BAADA YA MAOMBI, NAFASI YA MUNGU NA WEWE KTK UCHAGUZI NA MAISHA BAADA YA UCHAGGUZI.

@ “HUDUMA YA GOMBO LA CHUO” Tunawatakia watanzani wote uchaguzi mwema.
@ Daniel Mwaitenga.
Share:
Designed and Developed by Joel Elphas 0757 755 228 or 0655 755 228 © HUDUMA YA GOMBO LA CHUO ...Ukawaambie maneno yangu. Ezekiel 3:4 | ronangelo | NewBloggerThemes.com