... ukawaambie maneno yangu. Ezekiel 3:4

SEHEMU YA PILI: NAMNA YA KUJIUNGANISHA NA MUNGU KUPITIA SADAKA


SEHEMU YA PILI: NAMNA YA KUJIUNGANISHA NA MUNGU UTOAPO SADAKA

Bwana asifiwe wewe upendwae sana na Mungu

leo tuangalie "mambo ya kuzingatia utoapo sadaka ili kukutana na Mungu."

Kumbuka tu sadaka ni ibada ambayo inakufanya kukutana na Mungu au kuunganisha moyo wako hasa uitoapo sawa sawa na kanuni na utaratibu wa Bwana.

Moja, Fahamu kuwa utoapo sadaka kinacholengwa ni moyo wako, hivyo ni muhimu sana kuandaa moyo wako kabla ujafanya maamuzi ya kutoa sadaka. Kumbuka kuwa sadaka si kitu cha kwaida kama wengi wanavyo weza kufikiri, moja ya mambo yanayoweza kumfunga mtu mikokoni mwa Mungu au miungu ni sadaka, moja ya kitu kinachoweza kumtoa mtu mikononi mwa Mungu au miungu na sadaka.Yeroboamu akawaza moyoni mwake, “Sasa inawezekana ufalme ukarudi katika nyumba ya Daudi.Kama watu hawa watapanda kwenda kutoa dhabihu (sadaka) katika hekalu la Bwana huko Yerusalemu, mioyo yao itamrudia bwana wao, Rehoboamu mfalme wa Yuda. Wataniua mimi na kurudi kwa mfalme Rehoboamu.’’ Baada ya kutafuta shauri, mfalme akatengeneza ndama wawili wa dhahabu. Akawaambia watu,“Ni gharama kubwa kwenu kukwea kwenda Yerusalemu.Hii hapa miungu yenu, Ee Israeli, iliyowapandisha kutoka Misri.’’Ndama mmoja akamweka Betheli na mwingine Dani.Nalo jambo hili likawa dhambi, watu wakawa wanaenda hadi Dani kumwabudu huyo aliyewekwa huko.Yeroboamu akajenga madhabahu mahali pa juu pa kuabudia miungu na kuwateua makuhani kutoka watu wa aina zote, ijapokuwa hawakuwa Walawi. 1Falme 12: 26-31

Nachotaka uone hapo, ni njia ambayo Yeroboamu aliitumia ili kuvunja mahusiano ya hawa ndugu na Mungu aliye hai, alihusisha mambo makuu matatu, mioyo yao, sadaka, na miungu kupitia madhabahu alizo zitengeneza.Kumbuka kuwa biblia inasema hazina ya mtu ilipo ndipo na moyo wake utakuwepo, maana yake sadaka inauhusiano mkubwa sana na moyo, kuna uhusino mkubwa wa maendeleo ya moyo wako na mahusiano ya sadaka unayotoa; lakini pia

Mbili, Biblia inasema waambie wana Waisrael wanitolee sadaka kwa moyo wa kupenda, maana yake sadaka ni kipimo cha upendo wako wako mbele za Bwana, moyoni mwako kuna upendo wa Mungu kwa kiwango gani; ambacho kitadhirisha utayari wakujitoa kwaajili yake tena kwa furaha kwaajili ya kazi zake kwa kiwango gani,
Kwahiyo jambo hili linakupa kujua thamani ya Mungu maishani mwako, ambayo thamani hiyo italeta msukumo ndani ya moyo wako kutoa sadaka yenye thamani mbele zako na mbele za Mungu. kwahiyo Roho Mtakatifu anapoachilia msukumo wa wewe kutoa sadaka kiwango kile anachotaka, moyo uliandaliwa unakupa msukumo kutoa pasipo manung’uniko yoyote ila kwa furaha katika kile Mungu alicho kukilimia.Bwana akamwambia Musa,“Waambie Waisraeli waniletee sadaka. Utapokea sadaka kwa ajili yangu kutoka kwa kila mtu ambaye moyo wake wapenda kutoa.” Kutoka 25:1-2.  

Tatu, Kwa imani Abili alimtolea Mungu dhabihu bora zaidi kuliko Kaini. Kwa imani alishuhudiwa kuwa mwenye haki, Mungu mwenyewe akazishuhudia sadaka zake. Kwa imani bado ananena ingawa amekufa.Waebrania 11:4
Maana yake sadaka ni kipimo cha imani na imani ni mlango unaokupa haki mbele za Bwana. Kutoa sadaka ambayo ni zida kwa upande wako au yenye thamani upande wako na kumpa Mungu ni kipimo cha Imani yako. Mana Abali, alimpa Mungu vilivyo vinono, Ibrahimu alimpa Mungu Isaka mwanae wa pekee kama sadaka, Mama mjane alimpa Mungu senti iliyo onekana kubwa mana ndicho alicho kuwa nacho pekee kama sadaka n.k, kinacho pimwa hapo ni utayari, na imani waliyokuwa nayo. Ni eneo linalotupa fulsa ya kujua kuwa tutoapo sadaka, ni lazima kuiunganisha na imani mioyoni mwetu. Toa sadaka kwa imani kwamba kupitia sadaka hiyo utakutana na Mungu.

Nne, Sadaka ni kipimo cha kumcha Mungu, Mungu huifurahia zaka yako kwakuwa ni sehemu ya heshima unayo muoyesha mbele za macho yake. Thamani ya sadaka yako inabebwa na kiwango cha uchaji wa Mungu uliyomo ndani yako. Yani namaanisha hivi, utoapo sadaka Mungu anatazama ni kwa kiwango gani unamcha au kumuhofu yeye, kwasababu sadaka inatolewa kutokana na kanuni na maelekezo yake, kwahiyo kitendo cha wewe kutoa sadaka sawa sawa na maagizo yake ni ishara ya uchaji wako mbele zake, hivyo ni muhimu yeye kupitia sadaka hiyo kukuhudumia kwa ukaribu zaidi.

Hakikisheni mmetenga sehemu ya kumi ya mazao yote ya mashamba yenu kila mwaka.Mtakula zaka za nafaka yenu, divai mpya, mafuta na wazaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ng’ombe na ya kondoo na mbuzi mbele za Bwana Mungu wenu pale mahali atakapopachagua kama maskani kwa ajili ya Jina lake,ili kwamba mpate kujifunza kumheshimu/ kumcha Bwana Mungu wenu daima.”  Kumbukumbu 14:22-23
Au umesahau kuwa Ibrahimu alivyotii kumtoa Isaka sawa sawa na uataratibu wa Bwana biblia inasema Mungu alimwambi nimejua kuwa unamcha Mungu na sababu hiyo nitatimiza ahadi yangu juu yako na uzao wako. (Mwanzo 22: 12) Akamwambia, “Usimdhuru kijana,
wala usimtendee jambo lolote. Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwa sababu hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee.’’

Tano, Sadaka kwetu ni ukunjufu wa mioyo yetu mbele za Bwana, lakini pia ni mlango wa sisi kupokea kwa wingi au uchache, sawa na tuutoavyo mbele za Bwana “Lakini nasema neno hili;apandae haba atavuna haba; apandae kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu, ... Mungu humpenda yeye atoaye kwa ukarimu.”  2koritho 9:6-7

Haya ni mambo yanayo onesha nguvu iliyobebwa kwenye eneo la Sadaka, na mtu akiyazingatia atoapo sadaka ni lahisi sana kukutana na nguvu za Mungu.
Eneo la sadaka ni pana sana, na si kwamba unaweza kulitazama kwa jicho moja la upande wa kuunganishwa na Mungu tu, hapana kama utazamavyo upana huo, yivyo vivyo ni muhimu kutazama upande wa pili. Upande wa pili ni namna sadaka inavyoweza kuvuruga mahusiano yako na Mungu. katika ulimwengu tulio nao kama utacheza na sadaka zinazo tolewa kwa miungu yani waganga na wachawi,maisha yako yana kuwa hatarini sana na ili ufanikiwe upande huu ni kwanjia ya sadaka. Kwani hujawahi kuona familia inakufa mmoja baada ya mmoja kwa sababu ya kuotlewa sadaka, na anaefanya hivyo wengine wafe endapo atakosa sadaka miungu inamuuwa yeye mwenyewe, naamini umewahi kusikia.

Basi upande wetu tumuaminio Mungu sadaka nieno la muhimu sana kulijua, si eneo la utani kwa Mungu wetu. Si kama anashida sana na sadaka zetu, au kapungukiwa, la! Ila analinda na kupenda sana sadaka maana ni sehemu ya utukufu, na shukurani kwake. Biblia inaweka wazi AKani alilaaniwa sababu ya sadaka, manabii mianne walikufa kwanguvu iliyopitia kwenye sadaka, Anania na Safira mkewe walikufa kwa sababu ya sadaka, Akani alikufa kwa sababu ya vitu vilivyo kuwa vimewekwa wakfu kama sadaka ya Mungu, Nebukdreza alikolofishana na Mungu kwa sababu hiyo hiyo, na maeneo mengine mengi ambayo ukisoma biblia utayona yamewekwa wazi. Kwanini sadakja ili vunja mahusiano ya watu na Mungu kwa upana mkubwa hivyo? ni muhimu ujue kuna siri kubwa katika sadaka.

Ni sadaka ili muinua Ibrahimu mpaka kuitwa baba wa Imani,Ni sadaka ya nadhiri iliyo sababisha motto Samuel akapatikana, sadaka ili mkumbusha Mungu juu yam cha Mungu wake Kornelio, Sadaka ili pitisha nguvu ya Mungu na kumshindia Elia, sadaka ilikuwa harufu kwa Mungu pale Nuhu alipoitoa hata Bwana akaweka agano la kutokuuwa kwa mafuriko ulimwengu mzima. Nachotaka uone ni upana wa eneo hili la sadaka na mimi nimekufundisha kwa uchache sana kulingana na kipengere alicho nipa Roho Mtakatifu kukielezea. Lakini nakujengea kiu na msukumo wa kutamani kukutana na Mungu kupitia sadaka, ndio sadaka inaweza kuinua maisha yako katika Nyanja zote za maisha yako.

umebarikiwa sana na Mungu.
tutaendelea sehemu ya tatu...........

 ......."Mambo ambayo uaweza kupokea kutoka kwa Mungu kupitia sadaka"
@Huduma Ya Gombo La Chuo (Daniel Mwaitenga)
Share:

SEHEMU YA KWANZA: NAMNA YA KUJIUNGANISHA NA MUNGU KUPITIA SADAKA

NAMNA YA KUJIUNGANISHA NA MUNGU UTOAPO SADAKA.
Bwana asifiwe!!
Naamini upo tayari nikuletee somo hili,
Basi neema ya Yesu Kristo, Upendo wa Mungu Baba na Ushirika wa Roho Mtakatifu ukufunike,
Tutaangalia mambo makuu mawili
  1. Mambo ya kuzingatia utoapo sadaka ili kukutana na uwepo wa Mungu kupitia sadaka hiyo
  2. Mambo unayoweza kukutana nayo, kupata au kupokea utoapo sadaka. 

UTANGULIZI:
Nikweli kwamba 
moj; kushindwa kuona faida na maana ya kutoa sadaka kumesababisha Wakristo wengi kushindwa au kuchelewa kupokea mambo ya rohoni na mwilini sawa sawa na neno la Mungu liahidvyo, kwani si wengi wanapokea matunda ya kile wanachokitoa. Wengi wanajitahidi kutoa lakini bado milango haifunguki, kwa hiyo wanakuwa na maumivu mioyoni mwao nakukata tamaa kwenye eneo la utoaji,
Kitu cha pili wengi wanaamini sadaka wanayotoa wanakula watumishi au watu au inawatajirisha watumishi na wala haiendi popote, hasa wanapokutana na ugomvi unaotokana na sadaka makanisani n.k, kwa hiyo mzigo au msukumo wa kutoa sadaka miyoni mwao ni mdogo na kupelekea kutoa kama mazoea mana mioyoni mwao wanamtazamo na imani yakuwa zinaenda mifukoni mwa watu.

Nimuhimu sana ujue jambo hili, uwendapo mbele za Bwana ilikutoa na kupokea kuna kanuni na utaratibu wa Mungu mwenyewe ambao ni lazima ufahamu kinyume na hapo utoaji wako bado utakuwa na hasara, na mateso au maumivu ya upotevu wa mali yako. kweli bara tuelezane ukweli kuliko kukuacha utoe bila faida, hata neno la Mungu limeweka wazi jambo hili.

Lakini kadili unavyo soma kipengere hiki kuna ufahamu mpya Mungu atakusaidia kujua eneo hili, sadaka ni ibada kati yako binafsi na Mungu. Eneo la sadaka ni jambo la siri na binafsi kati yako na Mungu, kutoa sana au kidogo, kutoa kwa mchungaji au mtumishi Fulani bado havikusaidii kama ufahamu wako utaishia kujadili mambo hayo na kuyapa nafasi katika moyo wako.Lakini kulenga dhamira ya moyo wako sadaka unayotoa inaenda wapi na kwa nani (mtu au Mungu), imani yako katika sadaka utoayo, na uwaminifu wako mbele za Mungu ndio maana halisi ya sadaka yako. Kwa namna hii, naamini Mungu anataka ujue eneo la utoaji lilivyo na nguvu, lilivyo la muhimu na linavyoweza kukuunganisha na Mungu.

 Sijui kama unajua jambo hili, kuwa moja ya maeneo ambayo yanaweza kukuunganisha moyo wako au kukutoa mikononi mwa Mungu au miungu ni sadaka; pia ni eneo linaloweza kujenga au kuharibu mahusiano yako na Mungu au miungu. Awe ni Mungu au miungu pande zote hutaka na hutolewa sadaka, na maeneo yote yana kanuni amabazo zinataka kufanana.

Tufuatane pamoja kwa kusoma neno la Mungu, uone nacho zungumza nawe; Malaika wa Bwana alipomtokea Gideoni, akamwambia, “Bwana yu pamoja nawe, Ewe shujaa mwenye nguvu.” Gideoni akajibu, “Ee Bwana wangu, kama Bwana yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametutokea? Yako wapi basi yale matendo yake makuu baba zetu waliyotusimulia juu yake waliposema, ‘Je, Bwana hakutupandisha kutoka Misri? Lakini sasa Bwana ametuacha na kututia katika mkono wa Midiani.” Bwana akamgeukia na kusema “Enenda kwa uwezo wako huu, ukawaokoe Israeli kutoka mkononi mwa Wamidiani. Je, si mimi ninayekutuma wewe?’’ Gideoni akauliza, ‘‘Ee Bwana wangu, nitawezaje kuwaokoa Israeli?Ukoo wangu ndio dhaifu kuliko zote katika Manase, nami ndiye mdogo wa wote katika jamaa yangu.’’ Bwana akamjibu, ‘‘Nitakuwa pamoja nawe, nawe utawapiga Wamidiani kana kwamba walikuwa ni mtu mmoja.’’ Gideoni akajibu, ‘‘Kama basi nimepata kibali machoni pako, nipe ishara kuonyesha kweli kwamba ni Wewe unayesema nami.Tafadhali ninakuomba usiondoke hapa mpaka nitakaporudi na kukuletea sadaka yangu na kuiweka mbele yako.’’Naye Bwana akamwambia,‘‘ Nitangoja mpaka utakaporudi.’’ Waamuzi 6:12-22.

Natumai umewahi kuzisoma habari za Gidion zinazopatikana Sura hiyo ya 6, Lakini muhimu kwangu nataka tujue kwamba, wakati Mungu anamtokea Gidion, taifa la Israel lilikuwa mikononi mwa adui zao ambao ni Wamidiani. Taifa la Israel walikuwa wakivuna mavuno yao Wamidian wanachukua na mateso mengi waliyapitia mikononi mwa hao adui zao. Inawezekana na wewe unapita katika matatizo magumu, lakini kwanza nataka ujue wana waisrael walipita katika wakati mgumu sana, kosa lao lilikuwa ni kumuacha Mungu, Kumuasi na kutumikia miungu mingine, kwa muda mrefu Mungu aliwanyamazia kimya.

Mungu alipokusudia tena kuwarudia alijifunua kupitia kijana mmoja aliyekuwa wa familia iliyokuwa masikini na alikiuwa ni mtoto wa mwisho. Jambo kubwa lililokuwa katika ufahamu wa Gidioni ni kwamba, aliwahi pewa habari za ukuu wa Mungu jinsi na namna alivyo wakomboa baba zake kutoka Misri. Na swali kubwa alilokuwa nalo, ambalo nahisi ilikuwa ni shauku yake kuwa siku Bwana akitokea nita muuliza, na kweli sikumoja Mungu alijifunua mbele ya macho yake, Gideoni akasema, “Ee Bwana wangu, kama Bwana yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametutokea? Yako wapi basi yale matendo yake makuu baba zetu waliyotusimulia juu yake waliposema, ‘Je, Bwana hakutupandisha kutoka Misri? Lakini sasa Bwana ametuacha na kututia katika mkono wa Midiani.” (Waamuzi 6:12)
Ni ukweli wa dhati kuwa,kama umewahi sikia kwa watu kuwa Mungu anafanya mambo makuu lakini kwa wakati wako huyaoni na unateseka utakuwa na maswali zaidi kuhusu Mungu ukihusianisha na hizo habari ulizo ambiwa,ndivyo ilivyo kuwa kwa Gidioni, na jambo hilo lilimuumiza sana.
Nahisi atawewe unajambo ambalo kama Bwana angejifunua leo ungemuuliza, yawezekana lina kuumiza sana, tena kwa namna ulivyozipokea habari za Yesu, hukudhani kama jambo hilo lingeendelea kuwa gumu kiasi hicho, embu jifunze hapa namna Roho Mtakatifu alivyoamua kuingilia kwa Gidio ilikukuvusha na wewe;

(Naamini tuko pamoja, Kama ndio sema ndio, Kama sio Roho mtakatifu arudishe mawazo yako hapa ili upokee alichokusudia)
Nachotaka tujifunze ni namna Mungu alijifunua kupitia Gidioni ili kuliokoa taifa la Israel; na kitu cha msingi ndani yangu natamani ujue namna utukufu ule ulioshuka kwa Gidioni uliweza kuwa sehemu ya Gidioni miaka mingi kupitia nguvu ya kuoa Sadaka, sema tena nguvu ya Sadaka).
Gidioni alipata kibali mbele za Mungu, lakini shida kwake si kama alikuwa anataka kibali ila anachotaka ni uhakika wa taifa lake kuwa salama, na Mungu asingeweza kumtumia bila kibali, Gidioni akaamuwa kutafuta uhakika,uthibitisho wa kuwa Mungu atamtumia yeye na kuhakikisha wanatoka kwenye eneo linalo wasumbua.

Nisikie vizuri hapa, Si Malaika alimuomba Gidion sadaka, lakini Gidion alipoona Malaika amejifunua mbele yake alimuomba Malaika asiondoke mpaka amtolee sadaka,

 Malaika alifurahia na kuahidi kuisubili, ni msukumo wa ndani aliokuwa nao Gidion, tena ni siri ambayo Gidion alikuwa anajua, lengo la Gidioni ni kujiunganisha na Mungu kwa njia ya Sadaka, ili kuruhusu uthibitisho wa Mambo ya kimungu, pia ili kuruhusu kufuatiliwa na nguvu za Mungu. Biblia inadhihirisha nguvu iliyomo kwenye sadaka,

Tutaendelea Sehemu ya pili ya somo hili.
..... Mambo yakuzingatia utoapo sadaka"
@Huduma Ya Gombo La Chuo (Daniel Mwaitenga)
Share:

TAFAKARI LA WIKI 29/8/2015



UMEJIANFDAAJE”?

Matendo ya Mitume 7: 18 “Hata mfalme mwingine akainuka juu ya misri, asiye mfahamu Yusufu.”
 Tazama pamoja na mimi maneno haya; (MFALME MWINGINE), (MISRI) na (ASIYE MFAHAMU YUSUFU).
Kuna maneno ya msingi sana tuyatazama katika tafakari hili kupitia Matendo ya mitume 7:18, ni yamuhimu wewe kuyafahamu ya kupeleke kwenye lengo la tafakari letu, Kwanini imeandikwa “mfalme mwingine” …..(Misri)……. “asiye mfahamu Yusufu”
Ndugu wa Yusufu (familia ya Yakobo) wakiwa, utumwani(misri) waliishi katika mazingira mazuri sana, kwasababu Yusufu alikuwa kwenye utawala wa juu, pamoja nakuwa ni utumwani MUNGU alimpa kibali na akapewa wadhifa mkubwa sana.

Nielewe hivi, mfano; hata ukifanya kazi benki wakati huna elimu/ujuzi stahiki, ni sawa na mtu anayeishi utumwani, ni muhimu sana ujue yawezekana si kosa mana kwako ni muujiza, ila fanya maandalizi mana kuna siku utawala utabadilika. Au, yawezekana kuna kazi umepata, kama muujiza tu, au kwasababu wewe ni mzuri tu, au kwasababu ya umaarufu wa watu Fulani n.k; ila ukweli wa dhati kabisa elimu ya/ujuzi wa kazi hiyo hauna……..jiandae…..tena jiandae.

Kuna mabadiliko mbele sijui umejiandaaje, hata kama umeokoka wewe fanya maandalizi.
Muujiza huwa unakikomo (umejiandaaje baada ya muujiza huo kuisha), anakuja mtawala ambaye hana hobi ya kutazama uzuri wako kazini, au mtawala ambaye hajuani na huyo mtu maarufu aliyekufanya ukae hapo; wakati huo huyo mtu maarufu hayupo tena duniani.

Inawezekana haupo mahali sahihi lakini maisha yanaenda vizuri sana, sababu mtawala wa eneo hili amempa wadhifa mkubwa ndugu yako na ndugu yako akakufanya uishi maisha mazuri hapo. Lakini umejiaandaaje endapo ndugu yako akafa au akatolewa hapo na akainuka mfalme mwingine asiye mfahamu Yusufu( ndugu yako).
Mfano: huna elimu ya kufanya kazi benki, lakini unafanya kazi benki, kwasababu meneja aliopo anafahamiana na babayako, je, siku anakuja meneja mwingine “asiye mfahamu baba yako”, umejiaandaaje?
 (ukweli pamoja nakuwa umetoa ushuhuda kanisani kuwa Bwana ametenda kwa wewe kukaa nafasi ambayo kiuhalisia huna ujuzinayo, na sababu iliyokuweka hapo yawezekana ni kama muujiza au ni kibali na kujulikana kwake baba yako; …umejiaandaaje mpendwa?)

Wana wa Yakobo walipata wakati mgumu sana, wakati Yakobo amekufa, na Yusufu amekufa; mbaya zaidi ameinuka mfalme mwingine asiye mfahamu Yusufu; maisha yao yalibadilika kabisa, historia yao ilibadilika kabisa, kosa ni kwamba walifikiri kuwa milele Yusufu ataishi au milele Yule aliyempa yusufu nafasi ataishi.

Haijarishi umeokoka kiasi gani swala la wewe kuwa namaandalizi ya mabadiliko kwa mambo ya mbele na mabadiliko ya kiutawala ni muhimu sana. Haijarishi ni Mungu kakuweka hapo, swala la wewe kumuuliza Mungu mambo ya mbele na kumsihi kukuandaa kuyakabili na kuyashinda mabadiliko ni muhimu sana.
Ukipewa nafasi kwasababu Fulani ambayo kimsingi hukustahili, imepatikana kiujanja ujanja tu, au kwaneema tu au muujiza  ambao yawezekana lengo la Mungu wakati huo ni kukustili kwa wakati wakitambo kifupi tu, basi jifunze sana kujiandaa kwaajili ya kuimiliki na fasi hiyo kwa haki na ujuzi stahiki; ili kuyakabili mabadiliko yoyote ambayo kamwe hayata angalia umaalufu wa babayako,  ndugu zako, au uzuri wako.

@Daniel Mwaitenga.
Share:

HUDUMA YA GOMBO LA CHUO


Kwa kushirikiana na Kanisa la Moravian Sengerema..

Tunamshukuru Mungu wetu kwa Nguvu na Uweza kwa kutuwezesha Kuimaliza SEMINA ya Neno la Mungu katika eneo la Sengerema.
Ubarikiwe zaidi kwa maombi yako,kwani yamekuwa Manukato mazuri mbele za Mungu. 
Nasi tumeacha alama ya mbegu ya kiroho ambayo Mungu amepanda miyoni mwa kanisa lake, kwa kupanda miti katika ardhi hii. Mungu awabariki wote!!






Share:

NAMNA YA KUJIUNGANISHA NA NGUVU ZA MUNGU ILI ZIKUSAIDIE KATIKA NYANJA ZA MAISHA YAKO YOTE


UTUKUFU WA MUNGU UNAPOSHUKA, KUTAKA NGUVU ILIYO NDANI YA UTUKUFU HUO IKUSAIDIE WEWE, NI SUALA BINAFSI KATI YAKO NA MUNGU SIO WATU WENGINE, HATA KAMA UTUKUFU HUO UMESHUKA KATIKATI YA KUNDI.



Bwana Yesu Kristo asifiwe!!
iii / Mwendelezo……

Nimeshuhudia Semina nyingi, Mikutano mingi,matamasha ya Kusifu na Kuabudu, Ibada binafsi au zamakundi nyumbani au makanisani zikishamiri utukufu wa Mungu, lakini utukufu huo hautusaidii kwa kiwango kilicho kusudiwa mana unabaki kuwa ni wa mtumishi aongozae ibada hiyo au wa mahali pale ibada hiyo ilipofanyika, tunashindwa kwenda nao makazini ,majumbani mwetu au kuutumia katika maisha yetu ya kila siku.Nilitoa sababu na naendelea kuzungumza nawe namna tunaweza kukaa mkao ambao tutaufaidi utukufu wa Mungu mahali popote unaposhuka katka maisha yetu ya kila siku.

1.Jifunze kuutambua na tumia NGUVU ya Roho mtakatifu inayoshuka kwaajili ya kukuandaa kabla au wakati wa ibada; nguvu hiyo inakuwa na kusudi na nimuhimu kujua kwanini msukumo wa kujitakasa umeshuka kwa wakati huo, ukiwa barabarani,nyumbani,kanisani,kwenye gari,kazini n.k na nguvu hiyo inataka itumiwe ndani ya muda gani. "Nguvu YA MUDA WA TOBA NA UTAKASO.”
Mbeleni Mungu akinijalia, nitaelezea dondoo hii kwa undani,naamini itakusaidia.
Yoshua3:5 Ndipo Yoshua akawaambia hao watu, “JITAKASENI, kwa kuwa KESHO BWANA atatenda mambo ya kushangaza katikati yenu.”
Hapa Mungu alitaka kujufunua kwao si kwa mazungumzo la! Ila alitaka kwa kushusha utukufu wake awavushe mto yordani, ukiona Mungu amewapa masaa 24 ya kujitakasa ujue kuna sababu.

2. Nimuhimu sana, kufahamu kuwa unapoingia kwenye ibada unatakiwa kujiunganisha moyo wako na Madhabahu ya Mungu, na Mungu mwenyewe na Ufalme wa Mungu uliozamu kushuka na kuhudumia ibada hiyo.
Tazama kosa walilofanya hawa ndugu, la kijiunganishi na watumishi wa Mungu badala ya kujiunganisha na Mungu; Utukufu wa Mungu uliposhuka Ibada ikaisha wao wakabaki waanajadili lile wingu na kufikiri ni kina Paulo walifanya vile na kutaka kuwasujudia na kuwainua wao, jua,hawakufaidi chochote mpaka walipokemewa na kufundishwa,
Tazama Elimu ya kiroho MT.Paulo aliyowapa:-
Matendo ya mitume 14:15 “Enyi watu, kwa nini mnafanya mambo haya? Sisi ni wanadamu tu kama ninyi! Tunawaletea habari njema, tukiwaambia kwamba mgeuke mtoke katika mambo haya yasiyofaa mmwelekee Mungu aliye hai….”

3. Unapogundua utukufu wa Mungu umeshuka kwako katika namna ya pekee, jifunze kujiungamanisha na utukufu huo kwa SADAKA. Hiyo ni alama na njia inayolazimisha utukufu huo kukufuatilia hata baada ya ibada hiyo.
Waamuzi 6:18-22. 18 Tafadhali ninakuomba usiondoke hapa mpaka nitakaporudi na kukuletea sadaka yangu na kuiweka mbele yako.’’ Naye BWANA akamwambia, ‘‘Nitangoja mpaka utakaporudi.’’ Tumia SADAKA hiyo kuzungumza na Mungu- Mwanzo 18:1-8 Abrahamu akainua macho akaona watu watatu wamesimama karibu naye. Alipowaona, aliharakisha kutoka kwenye ingilio la hema lake kuwalaki na kuwasujudia hadi nchi. 3.Akasema, “Kama nimepata kibali machoni penu, ee bwana wangu, usimpite mtumishi wako. 4Acha yaletwe maji kidogo, kisha ninyi nyote mnawe miguu yenu na mpumzike chini ya mti huu. 5Niruhusuni niwapatie chakula kidogo mle, ili mpate nguvu mwendelee na safari yenu, kwa kuwa mmekuja kwa mtumishi wenu.’’ Nao wakamjibu, “Vema sana, fanya kama unavyosema.’’

4. Wakati huo utukufu wa Mungu unashuka, omba roho ya Mungu iliyomo ndani ya huo utukufu ikae juu yako, kabla hujafikiri kuomba mahitaji yako. Hesabu 11:25, 2Falme 2:9. “…Elisha akajibu, “Naomba nirithi sehemu maradufu ya roho yako.’’ Kumbuka ndugu; kitendo cha Elisha kuomba ile roho si roho ya Elia ila roho wa Mungu aliye kuwa juu ya Elia. Vivyo hivyo roho ya Mungu iliyo kuwa juu ya Musa kwa wale watu 70. Sasa kumbuka mabadiliko makubwa ambayo yalifanyika pindi roho hiyo ilipo kaa ndani yao.

5.            Uwe mwenye  kutamani kusikia na kuelewa/kujua na kuamini ujumbe uliobebwa kwenye huo utukufu;  utukufu wa Mungu ukishuka unakuwa na ujumbe au sababu ya kushuka hapo; kumbuka neno la Mungu ndio ujumbe unaobebwa katika utukufu huo, ndio majibu yanayokujia,na ndio hatua ya imani yako. na maadamu ukiamini umeshuka mahali ulipo lazima ujue unakuhusu na wewe.5.         Weka IMANI kubwa kwa Mungu aliyejifunua hapo na  kwa yale unayoenda kuyaomba.
Marko 9:22-24 …………………Lakini kama unaweza kufanya jambo lo lote, tafadhali tuhurumie utusaidie.’’ 23Yesu akamwambia, “Kama ukiweza kuamini, yote yawezekana kwake yeye aaminiye.’’24Mara baba yake yule mvulana akapiga kelele akisema, “Ninaamini. Nisaidie kutokuamini kwangu!’’

7.            Achilia mahitaji yako kwa kadiri Roho Mtakatifu anavyo kusukuma kuomba, kwa lugha nyepesi huo ni muda mzuri wa kujiachia kuzungumza na Mungu, mana amejifunua, Roho Mtakatifu anaweka ajenda za muhimu,za lazima na za muda sahihi ndani yako zinazo kuwa na mahusiano makubwa na maisha yako ya sasa na baadae katika kusudi uliloumbiwa (future yako) ambazo ni muhimu uzungumze na Mungu kwa mzigo na msukumo wa maombi mahali hapo. Kumbuka habari za Bartimayo Kipofu, mama mwenye kutokwa damu miaka 12  (Marko 5:25-34), Musa alivyo kuwa anajiachilia mbele za Bwana na taifa lake pia (Kutoka 24:10-25).

8.            Ili kumiliki utukufu wa Mungu ulioshuka,hasa ukusaidie baadae, jitahidi sana kuwa mchunguzi wa neno la Mungu na mtii wa kila utakacho kielewa kwa kwa kukitenda Hivyo ni muhimu wingu hilo unapofika katika utulivu kuwa mchunguzi wa neno lililo achiliwa wakati huo.
Matendo ya Mitume  17:11-12 “Hawa Wayahudi wa Beroya walikuwa waungwana zaidi kuliko wale wa Thesalonike,kwa kuwa walilipokea neno lile kwa uelekevu wa moyo,wakayachnguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo 12Wayahudi wengi wakaamini pamoja na wanawake na wanaume wa Kigiriki wa tabaka la juu.”


@Daniel Mwaitenga.
Huduma Ya Gombo La Chuo.
Share:
Designed and Developed by Joel Elphas 0757 755 228 or 0655 755 228 © HUDUMA YA GOMBO LA CHUO ...Ukawaambie maneno yangu. Ezekiel 3:4 | ronangelo | NewBloggerThemes.com